Pata taarifa kuu

Uganda na Tanzania zafikia makubaliano mradi wa Bomba la mafuta

Makampuni ya mafuta ya Ufaransa TotalEnergies na China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) kutoka China, zimetia saini mkataba wa Dola Bilioni 10 kujenga miundo mbinu za kuwezesha kusafirisha mafuta kupitia nchini Tanzania, mradi ambao umeshtumiwa na wanaharakati wa mazingira.

Rais wa Uganda akitia saini kwenye bango wakati wa hafla ya kutia saini mradi mkubwa wa mafuta mjini Kampala, Februari 1, 2022.
Rais wa Uganda akitia saini kwenye bango wakati wa hafla ya kutia saini mradi mkubwa wa mafuta mjini Kampala, Februari 1, 2022. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Madhumuni ya makubaliano haya, yanayoitwa Uamuzi wa Mwisho wa Uwekezaji, kufikia uzalishaji wa mapipa 230,000 kwa siku ifikapo 2025 ni mradi mkubwa unaoendelea kuzua utata nchini Uganda.

Makubaliano yaliyofikiwa yanafanya kuanza kwa mradi wenyewe. 

Mradi huu mkubwa utajikita na uchimbaji wa mamia ya visima vya mafuta kwenye mwambao wa Ziwa Albert, na ujenzi wa bomba la mafuta linalounganisha Uganda na Tanzania.

Pesa zilizowekezwa Jumanne na kampuni za TotalEnergies na CNOOC zitazindua ujenzi wa mradi huo na zinaweza "kukuza uchumi", alisema Rais Yoweri Museveni ambaye alipuuzilia mbali ukosoaji kutoka kwa mashirika yasio ya kiserikali juu ya hatari ya mazingira.

Mashirika yanayokemea mradi huu ni watu ambao hawana kazi. Hawana la kufanya, waache wajinga hawa waendelee kuzurura hovyo, wanapenda tu kunywa chai na kula kaki. 

Mashirika yasiyo ya kiserikamli yamekosoa "athari" kwa sayari kutokana na mradi huu wa mafuta ambao utaathiri Hifadhi kadhaa za Asili.

"Tumeona kilichotokea kwa wakazi wa eneo hilo. Tumeona jinsi baadhi ya ardhi zilivyochukuliwa. Na wengine bado wanasubiri fidia. Kwa hiyo tuko makini sana. Serikali na kampuni za mafuta wawe makini zaidi. Je, fedha hizi zitakazoingizwa zitagawanywa vipi? Je, itabadilisha maisha ya wenyeji? Mkataba huu lazima utoe faida. Ni lazima utoe ajira, na fedha kwa vijana wetu. Na kisha kuna suala la mazingira, " amesema Richard Orébi, mwanaharakati wa Uganda kutoka shirika lisilo la kiserikali la Global Right Alert.

Siku ya Jumanne, Mkurugenzi wa kampuni ya TotalEnergies, Patrick Pouyanné, alijaribu kumaliza utata huo. "Tunafahamu umuhimu wa maeneo ambayo tutafanyia kazi, hasa kuhusiana na mazingira. "

Mwezi Desemba mwaka uliyopita, kampuni ya Ufaransa, iliyojiita TotalEnergies mwaka 2021, ilishtakiwa na mahirika yasio ya kiserikali ya Ufaransa na Uganda kwa kushindwa kuzingatia majukumu yake ya ulinzi wa mazingira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.