Pata taarifa kuu
UGANDA-DIPLOMASIA

Uganda na Rwanda zajaribu kuweka kando tofauti zao kuelekea kufufua uhusiano wao

Kamanda wa majeshi ya nchi kavu wa Uganda ambaye pia ni mtoto wa rais Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba amefanya ziara ya siku moja nchini Rwanda na kufanya mazungumzo na  rais Paul Kagame. 

Kamanda wa majeshi ya nchi kavu wa Uganda, Yoweri Museveni, Luteni Jenerali  Muhoozi Kainerugaba.
Kamanda wa majeshi ya nchi kavu wa Uganda, Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba. AFP - PETER BUSOMOKE
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Uganda inasema Kainerugaba alitumwa na rais Museveni kwenda kuzungumzia operesheni za jeshi la Uganda nchini DRC, lakini pia kuangalia uwezekano wa mpaka wa nchi hizo mbili kufunguliwa. 

Nchi hizi mbili zimefunga mipaka yao kutokana na kila upande kushtumu mwingine kuunga mkono na kusaidia waasi.

Mbali na Jenerali Kainerugaba, mjumbe mwingine wa Uganda Balozi Adonia Ayebare amefanya ziara nchini Rwanda. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.