Pata taarifa kuu
TANZANIA-USALAMA

Tanzania yataka kuepuka kuwasili kwa makundi ya kigaidi kutoka Cabo Delgago

Marais wa nchi Tanzania na Msumbiji walikutana Pemba, mji mkuu wa jimbo la Cabo Delgado kujadili mapambano dhidi ya jihadi. Jimbo hili lililo kaskazini mwa Msumbiji, linalopakana na Tanzania, limekuwa likikumbwa na ghasia za wanajihadi tangu mwishoni mwa mwaka wa 2017. Mkutano ambao haukutarajiwa Ijumaa hii, Januari 28 kati ya viongozi wa Msumbiji na Tanzania.

Wanajeshi wa Msumbiji na maafisa wa polisi wa Rwanda Septemba 24, 2021 huko Pemba katika jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji.
Wanajeshi wa Msumbiji na maafisa wa polisi wa Rwanda Septemba 24, 2021 huko Pemba katika jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji. AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

"Tuna tatizo la moja," Rias wa Msumbiji Filipe Nyusi alisema baada ya mkutano na mwenzake wa Tanzania. Nchi hizo mbili zina mpaka wa pamoja ambao una urefu wa zaidi ya kilomita 750 na ambao "magaidi huvuka", aliongeza.

Kwa muda wa miaka minne, makundi yenye silaha ambayo yameahidi utiifu kwa kundi la Islamic State yamekuwa yakihangaisha jimbo la Cabo Delgado. Mnamo mwaka wa 2021, walifikia hatua ya kuchukua udhibiti wa jiji la bandari la Palma, na kuzorotesha mradi mkubwa wa gesi - wenye thamani ya euro bilioni kadhaa. Katika miezi ya hivi karibuni, Rwanda na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wametuma zaidi ya wanajeshi 3,000 kusaidia jeshi la Msumbiji kuleta utulivu katika eneo hilo na kuzuia mzozo kusambaa.

Lakini Tanzania inahofia kuenea kwa vurugu. Mwishoni mwa mwaka wa 2020, mji wa Mtwara nchini Tanzania pia ulilengwa na mfululizo wa mashambulizi. Kwa upande wa Dodoma, wanasema ni muhimu zaidi kuulinda mpaka huu kwani rasilimali kubwa ya gesi imegunduliwa katika mkoa huu, ambao Rais Samia Suluhu anakusudia kuutumia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.