Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Marekani bado yamsaka Joseph Kony, kiongozi wa LRA

Kitita cha dola Milioni 5, kimetengwa kwa mtu yeyote atakayetoa habari zitakazowezesha kukamatwa kwa Joseph Kony. Ni taarifa iliyotolewa na balozi za Marekani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan ambayo inatukumbusha kuwa Marekani haijamsahau kiongozi wa Lord's Resistance Army, LRA.

Joseph Kony, kiongozi wa LRA.
Joseph Kony, kiongozi wa LRA. Reuters/Stuart Price/Pool
Matangazo ya kibiashara

Marekani imekuwa ikimtafuta Joseph Kony kwa muda mrefu, zaidi ya miaka 13 sasa. Ilikuwa katika majira ya kiangazi mwaka 2008 ambapo kiongozi wa Lord's Resistance Army (LRA) aliwekwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya marekani kwa ugaidi au uhalifu wa kivita.

Orodha hii ilitangazwa na rais Bush mara tu baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001. Baadaye, utawala wa Obama ulitumia karibu dola milioni 800 kuwawinda wanachama wa wanamgambo hao wenye jeuri na itikadi kali wanaojulikana kuajiri watoto askari na kuwabaka watu wengi. Lengo kuu la LRA lilikuwa ni kumpindua rais Museveni wa Uganda na kuanzisha utawala unaozingatia Amri Kumi za Mungu.

Kundi hilo ambalo linaendelea kusakwa, limesalia katika nchi kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Sudan Kusini. Operesheni ya Marekani ilimalizika mwaka wa 2017 baada ya kuona kuwa LRA tayari imeng'olewa meno.

Wapiganaji wake walibaki hadi mia moja. Wengi wameachana na kundi hilo. Wengine wamekamatwa na kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Dominic Ongwen, mmoja wa wanajeshi watoto wa Joseph Kony, ambaye bado hajapatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.