Pata taarifa kuu
RWANDA-USHIRIKIANO

Tanzania na Rwanda watia saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anaanza Jumanne hii, Agosti 3, siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake rasmi nchini Rwanda. Alipokelewa jana na mwenzake Paul Kagame katika ikulu ya rais.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. STR AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kwanza ya rais Samia Suluhu Hassan nchini Rwanda baada ya mtangulizi wake John Magufuli kuzuru nchi hiyo kabla ya kifo chake, mwezi Machi. Nchi hizo mbili zina uhusiano mzuri.

Ziara ya rais wa Tanzania nchini Rwanda inalenga"kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili," amesema Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Alikaribishwa Jumatatu na shangwe kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali, kisha akakutana na mwenzake Paul Kagame uso kwa uso. Wakati huo huo marais hao wawli walitia sani kwenye makubaliano mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano wa iuchumi, kama teknolojia ya habari, uhamiaji, elimu na udhibiti wa bidhaa za matibabu.

Ikiwa Paul Kagame alimwalika rais wa Tanzania kuja kuizuru Rwanda, kwanza ni kutaka "kupata washirika wapya kati ya majirani zake.

Wakizungumza na waandishi wa habari, baada ya kikao chao cha faragha, Rais Paul Kagame ameiahidi Tanzania kuwa Rwanda iko tayari kutoa ushirikiano kwa lolote ambalo linalenga maslahi ya pande mbili, ikiwemo kutafutia ufumbuzi matatizo yaliyotokana na janga la COVID-19.

Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza Rwanda kwa hatua iliyopiga katika sekta ya uchumi na mapambano dhidi ya COVID-19.

Na niwapongeze Rwanda kwamba mko mbele yetu nasi tuko tayari kuja kujifunza kwenu, lakini yapo mambo ambayo yameingia sasa ya Covid-19, nayo tumeyazungumza kwa mapana yake, na tumeweka mikakati ya kushirikiana kupitia kituo chetu cha Rusumo lakini pia kama tulivyosaini mambo ya madawa. Tumekubaliana kuendeleza ushirikiano uliopo ambao ni ushirikiano wa kihistoria na wa kindugu. Asanteni sana.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.