Pata taarifa kuu
TANZANIA-USHIRIKIANO

Samia Suluhu azuru Rwanda na kutia saini mikataba mbalimbali na mwenyeji wake

Rais wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan yupo nchini Rwanda ziara ya siku mbili  ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuingia madarakani mwezi Mei.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. © https://www.ikulu.go.tz/
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuwasili jijini Kigali, viongozi hao wawili wamejadiliana na kutiliana saini kuhusu ushirikiano wa masuala ya kiuchumi na teknolojia yanayolenga kuimarisha mahusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Naye rais Kagame amesema, ni muhimu kwa mataifa hayo mawili na mengine kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza ushirikiano hasa dhidi ya kushinda janga la Covid 19.

Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni alizuru Kenya, Uganda na Burundi na sasa ana zuru Rwanda kwa lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo na Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.