Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-UNICEF

UNICEF yasema Mamilioni ya watoto wanahitaji msaada nchini Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa watoto zaidi ya Milioni NNE wanahitaji msaada wa dharura kutokana na mzozo wa muda mrefu nchini Sudan Kusini.

Watoto wanaopitia maisha magumu nchini Sudan Kusini
Watoto wanaopitia maisha magumu nchini Sudan Kusini REUTERS/Kate Holt/UNICEF
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la watoto UNICEF, taifa hilo ambalo linaadhimisha miaka 10 baada ya kupata uhuru, Julai 9, 2011, linaendelea kukabiliwa na mizozo mibaya zaidi ya kibinadamu duniani.

Aidha, Shirika hilo la linaonya kuwa maisha ya watoto nchini humo ni taabu sana kwa sababu maisha yao yameendelea kukumbwa na machafuko.

Umoja huo umeongeza kusema kuwa maisha ya watoto wengi nchini humo ni ya tabu mno kwani bado wanakumbwa na ghasia, utapia mlo na changamoto mbalimbali.

Rais Salva Kiir na Makamu wa kwanza wa rais Riek Machar wameungana kutekeleza makubaliano ya mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.