Pata taarifa kuu
SUDANI YA KUSINI-SIASA

Umoja wa Mataifa watilia shaka utekelezaji wa mkataba wa Amani wa Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, unasema nchi hiyo bado iko nyuma katika utekelezaji wa mkataba wa Amani, huku suala la uundwaji wa jeshi la kitaifa likisalia kuwa tete.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akiwa na Riek Machar (kulia) Februari 20, 2020 huko Juba.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akiwa na Riek Machar (kulia) Februari 20, 2020 huko Juba. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe maalumu wa UN kwa nchi ya Sudan Kusini, Nicolas Haysom, amesema kiujumla utekelezwaji wa mkataba wa Amani unaenda taratibu, wakati huu rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wakijaribu kutengeneza jeshi la pamoja.

Wacdadisi wa mambo nchini Sudan Kusini wanahisi kuwa matamshi ya umoja wa mataifa yamekuja kwa kuchelewa kwa sababu baadhi ya wanasiasa waliona hakuna utashi wowote kwa upande wa serikali ya Salva Kiir kwa kufikia uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Wakili Ojwang Agina ni mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa jijini Nairobi anasema upande wa Kiir ulijipanga tangu mwanzo katika kuhakikisha mchakato huo haufikii malengo yake.

Hata hivyo baadhi ya maafisa wa umoja wa mataifa wanahisi kuwa juhudi za kimataifa zinahitajika katika kuzipatanisha pande hasimu katika taifa hilo dogo na changa la Afrika mashariki.   

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.