Pata taarifa kuu
KENYA - USAFIRI

Kenya Airways yasitisha safari za ndege kuelekea Uganda

Shirika la ndege la Kenya Airways, limesitisha safari za ndege kuelekea Entebe, nchini Uganda, kufutia hatua ya taifa hilo kuendelea kusajili idadi ya juu ya vurusi ya corona.

Ndege ya shirika la Kenya Airways
Ndege ya shirika la Kenya Airways REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Kenya Airways inajiunga na mashariki mengine ya ndege ambayo tayari yamesistisha safari za ndege kuelekea uganda, kama vile Rwanda Air na Emirates Airline.

Hata hivyo mkurugezi wa mawasiliano wa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini Uganda, UCAA, Vianney Luggya, amesema hawajapokea habari kuhusiana na hatua hiyo ya serikali ya Kenya, japo akakiri kupungua kwa safari za ndege kutoka Kenya.

Luggye pia ameongeza kuwa serikali ya Uganda imesitisha safari za ndege kutoka nchini India ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona.

Shughuli za kawaida nchini Uganda zimesitishwa kwa muda ili kuzuia maambukizi zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.