Pata taarifa kuu
Uganda - USALAMA

Uganda – Washukiwa zaidi wa jaribio la mauwaji ya waziri Wamala wakamatwa

Polisi nchini Uganda wamewakamata washukiwa 4 zaidi wa jaribio la mauwaji ya waziri wa uchakuzi Katumba Wamala, ambapo washukiwa hao walifanikiwa kumuua bintiye na dereva wake.

Polisi wa Uganda wawakamata watu 4, wanaoshukiwa kushiriki kwa njama ya kumuua m waziri wa uchukuzi Wamala
Polisi wa Uganda wawakamata watu 4, wanaoshukiwa kushiriki kwa njama ya kumuua m waziri wa uchukuzi Wamala Reuters/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Mshukiwa moja hata hivyo, ameuawa na polisi baada ya kukataa kukamatwa.

Kwa mjibu wa polisi washukiwa hao wamepokea mafunzo ya jeshi kama waasi katika taifa jirani la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kwamba walikuwa njama ya kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

Silaha kadhaa zimepatikana na washukiwa hao ikiwemo vifaa vya kujitengenezea bomu ya nyumbani.

Rais Yoweri Museveni, alitoa agizo kwa polisi kuhakikisha waliohusika katika jaribio hilo la mauwaji ya waziri kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.