Pata taarifa kuu
BURUNDI - SIASA

Burundi yaadhimisha miaka 59 ya uhuru

Nchi ya Burundi hii leo imeadhimisha kumbukumbu ya miaka 59 tangu pale ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Mkoloni Mbelgiji.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye awasili kwa ajili ya uzinduzi wa kutoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 3,000 katika jela kuu la Mpimba, kama sehemu ya juhudi za kupunguza msongamano katika magereza, Bujumbura, Burundi Aprili 26, 2021.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye awasili kwa ajili ya uzinduzi wa kutoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 3,000 katika jela kuu la Mpimba, kama sehemu ya juhudi za kupunguza msongamano katika magereza, Bujumbura, Burundi Aprili 26, 2021. REUTERS - EVRARD NGENDAKUMANA
Matangazo ya kibiashara

Sherehe za mwaka huu wa 59 zimehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadera waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na muakilishi wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta .

Kubwa zaidi ni uwepo wa waziri mkuu wa Rwanda katika sherehe hizo, Edouard Ngirente ambae alimwakilisha rais wa Rwanda Paul Kagame.

Rais Evariste Ndayishimiye amepongeza hatuwa hiyo na kueleza matumaini yake kuona Burundi na Rwanda zinafungua ukurasa mpya.

Sherehe hizo zinafanyika wakati huu kukiwa na minong’ono miongoni mwa wananchi wa taifa hilo hususan katika jiji la Bujumbura ya kubomoa majumba yaliojengwa kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.