Pata taarifa kuu
BURUNDI-

Burundi yamkumbuka Pierre Nkurunziza

Wananchi wa Burundi wanaadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha rais wao hayati Pierre Nkurunziza aliyeaga dunia Juni 8, 2020 katika hospitali kuu ya Cinquantennaire mkoani Karusi, katikati mwa Burundi, baada ya kuuguwa kwa muda mfupi. Pierre Nkurunziza alifariki dunia  kwa mshtuko wa moyo, kulingana na taarifa iliyotolewa na serikali wakati huo.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Juni 7, 2018.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Juni 7, 2018. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Burundi ilitangaza kifo cha Rais Pierre Nkurunziza, katika ujumbe ulioandikwa katika mtandao wa Twitter, uliosema kwamba Juni 8 "Timu ya madaktari walishindwa kunusuru maisha yake baada ya kupata mshutuko wa moyo."

Wasifu wa Pierre Nkurunziza

Pierre Nkurunziza alikuwa mwanasiasa wa Burundi na kuwa madarakani tangu mwaka 2005.

Bwana Nkurunziza, kijana wa aliyekuwa mbunge, alinusurika mauaji ya mwaka 1993 ya wanafunzi kutoka kabila la Kihutu katika Chuo Kiuu cha Burundi (UB) ambapo alikuwa mhadhiri na kujiunga na waasi wa kundi la FDD, kundi ambalo baadae lilibadilika na kuwa chama tawala cha CNDD-FDD ambacho alikuja akawa kiongozi.

Alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, hadi alipochaguliwa kama rais wa Burundi mwaka 2005.

Jeneza la Pierre Nkurunziza wakati wa mazishi yake katika uwanja wa mpira wa Gitega, Burundi, Juni 26, 2020.
Jeneza la Pierre Nkurunziza wakati wa mazishi yake katika uwanja wa mpira wa Gitega, Burundi, Juni 26, 2020. TCHANDROU NITANGA / AFP

Utata kuhusu muhula wa tatu wa Nkurunziza

Baada ya makubaliano ya Amani ya Arusha kati ya serikali na waasi, Nkurunziza alitajwa kuwa waziri wa utawala bora kabla ya bunge kumchagua kama rais Agosti 2005.

2015, Nkurunziza alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na utata na chama chake kwa muhula wa tatu madarakani.

Wafuasi wake na wanaompinga Nkurunziza walikosa kukubaliana katika suala la ikiwa ilikuwa halali kwake kugombea tena na maandamano yakafuata.

Zaidi ya miezi miwili kulitokea maandamano ya kumpinga Nkurunziza ambayo yaliandamana na ghasia na kusababisha vifo vya watu.

Mei 13, 2015, jaribio la mapinduzi dhidi ya Nkurunziza lilitokea akiwa nje ya nchi hiyo.

Mkuu wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare alidai kwamba amemng'oa mamlakani Nkurunziza lakini wanajeshi watiifu kwa Nkurunziza walikanusha madai hayo. Nkurunziza ameongoza taifa hilo kwa miaka 15.

Evariste Ndayishimiye (kushoto), anayeonekana hapa kwenye picha na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kabla ya kifo chake, wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2020.
Evariste Ndayishimiye (kushoto), anayeonekana hapa kwenye picha na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kabla ya kifo chake, wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2020. AFP

Nkurunziza alipaswa kukabidhi madaraka

Rais Pierre Nkurunziza aliyezaliwa Desemba 18, 1963 alikuwa ameratibiwa kumkabidhi mrithi wake madaraka jenerali Evariste Ndayishimiye.

Kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi ya Burundi, katika uchaguzi uliofanyika Mei mwaka 2020 mgombea wa chama tawala cha CNDD-FDD, Everiste Ndayishimye, ndiye aliyetambuliwa kuibuka na ushindi, hivyo basi, Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza alitakiwa kumkabidhi madaraka.

Juni 13, 2020, Rais mteule Evariste Ndashimiye atia saini kitabu cha wazi cha rambirambi kwa mtangulizi wake Pierre Nkurunziza, aliyefariki dunia, Juni 8.
Juni 13, 2020, Rais mteule Evariste Ndashimiye atia saini kitabu cha wazi cha rambirambi kwa mtangulizi wake Pierre Nkurunziza, aliyefariki dunia, Juni 8. Tchandrou NITANGA / AFP

Siasa za Pierre Nkurunziza

Mwaka 2015, rais huyo aliyekuwa na miaka 51-aliyeingia madarakani baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha mauaji ya watu 300,000, alisema kuwa hatawania tena nafasi hiyo ya urais kwa sababu ni kinyume na katiba.

Wafuasi wake walitetea kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2005 alichaguliwa na bunge na sio wapiga kura- na kutetea hoja hiyo katika mahakama ya katiba ya nchini humo.

Na kiongozi wa zamani wa waasi alimsifia kuwa kiongozi huyo ameleta amani katika utawala wake nchini Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.