Pata taarifa kuu
UGANDA-COVID 19

Uganda "yafungwa" kutokana na ongezeko la maambukizi ya Covid 19

Maafisa wa usalama nchini Uganda wameonekana wakipiga doria katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kuhakikisha kuwa masharti mapya ya kupambana na ongezeko la maambukizi ya Covid 19, yanatekelezwa.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni AP - John Muchucha
Matangazo ya kibiashara

Polisi  jijini Kampâla wamewafukuza wachuuzi katika barabara za jiji hilo siku ya Jumamosi  na kuwataka kurudi nyumbani.

Safari za abiria kati ya Wilaya za nchi hiyo zimezuiwa, usafiri wa umma umepigwa marufuku huku muda wa watu kutotembea nje sasa ukianza kati ya saa moja jioni mpaka saa kumi na moja na nusu Alfajiri.

Huduma zote za usafiri wa umma zimesitishwa,” amesema rais Museveni wakati akiwahotubia wananchi wa Uganda kupitia Televisheni Ijumaa usiku.

Hatua hizi zitadumu kwa wiki sita:

Mwaka uliopita, Uganda ilichukua masharti magumu ya kuwazuia watu kutembea wakati ilipokuwa na visa vichache na nchi hiyo ikafunguliwa tena baada maambukizi kushuka.

Madaktari wameliambia Shirika la Habari AFP kuwa hospital nchini humo zinakabiliwa na uhaba wa hewa aina ya Oxygen kutoka na wagonjwa wengi wanaokwenda hospitalini.

Kipindi cha wiki tatu zilizopita, maambukizi yameongezeka kutoka 100 kwa siku mpaka 1,700 licha ya hatua zilizochukuliwa wiki iliyopita, kufunga Shule, maeneo ya burudani na kuzuia mikusanyiko ya watu.

Tangu kuzuka kwa maambukiz ya Covid 19 mwaka uliopita, Uganda imeripoti maambukizi 70,893 na vifo  582 huku jiji kuu Kampala likiathiriwa zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.