Pata taarifa kuu

Rais wa Tanzania awasili nchini Kenya

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewasili nchini Kenya, kwa ziara ya siku mbili, ziara ambayo inatazamwa na wadadi wa mambo kama kiungo muhimu katika kujaribu kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alipowasili nchini Kenya kwa ziara ya kikazi.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alipowasili nchini Kenya kwa ziara ya kikazi. © StatehouseKenya
Matangazo ya kibiashara

Hii inakuwa ziara yake ya pili nje ya nchi ya Tanzania, ambapo mwezi uliopita, alifanya ziara nyingine nchini Uganda, ambako alikutana na mwenyeji Wake rais wa Uganda, Yoweri Museveni, na kutiliana saini mkataba wa kuanza ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi.

Ziara yake nchini Kenya, inafanyika wakati ambapo kwa muda sasa nchi hizo mbili zimekuwa zikitofautiana kwenye baadhi ya masuala ikiwemo biashara na namna ya kukabiliana na janga la Covid 19.

Mara ya mwisho kwa rais wa Tanzania kufanya ziara nchini Kenya ilikuwa ni miaka mitano iliyopita.

Akiwa nchini humo, rais Samia, atakutana na mwenyeji Wake rais Uhurua Kenyatta, ambapo baadae atalihutubia bunge kabla ya kufanya kikao na wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania.

Haya yanajiri wakati huu, wizara ya afya nchini Tanzania, ikitoa mwongozo mpya kuhusu ugonjwa wa Covid 19, ambapo sasa wageni na wenyeji wanaoingia nchini humo, watalazimika kuwa na cheti cha kuthibitisha kutokuwa na maambukizi.

Aidha watatakiwa kupimwa tena kabla ya kutakiwa kujitenga kwa siku 14 hasa kwa abiria wanaotokea kwenye nchi ambazo zina maambukizi ya juu pamoja na aina mpya ya virusi vya Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.