Pata taarifa kuu
RWANDA

HRW yashtumu hatua za rais wa Rwanda dhidi ya watumiaji wa Youtube

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch, limeishtumu Rwanda kwa kuendelea kubana, kuwatishia na kuwakamata wanaotumia mitandao ya Youtube na Blogu mbalimbali kujadili masuala mbalimbali nchini humo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (picha ya kumbukumbu).
Rais wa Rwanda Paul Kagame (picha ya kumbukumbu). SIA KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch inasema, hatua hii imekuja baada ya uongozi wa Kigali kuminya uhuru wa watu kujieleza kupitia vyombo vya Habari.

Shirika hilo sasa linataka viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Madola, watakaoshiriki kwenye kikao chao mwezi Juni, waishinikize Rwanda kufanya mageuzi muhimu ya kulinda uhuru wa kujieleza.

Aidha, ripoti ya Shirika hilo inaleza kuwa watu wanane ambao wamekuwa wakijadili au kutoa maoni kuhusu athari za hatua zilizochukuliwa kudhibiti maambukizi ya Covid 19, wamekamatwa, kutishwa na kuteswa kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Innocent Bahati, mwenye umri wa miaka 31 mwanamuziki ambaye amekuwa akikosoa serikali, ametoweka tangu mwezi Februari 7 mwaka huu.

Watu wanne, waliokuwa wanachambua matukio ya nchi hiyo kupitia Youtube, walikamatwa mwezi Aprili 2020, watatu walifunguliwa mashtaka na kuachiliwa huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.