Pata taarifa kuu
RWANDA

Rwanda: Kampeni ya chanjo dhidi ya COVID-19 yaendelea

Zaidi ya watu 250,000 walipokea dozi ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 nchini Rwanda kwa wiki moja, licha ya baadhi ya nchi kusitisha zoezi hilo.

Wahudumu wa afya wa kituo cha matibabu cha Biomedical Center Kigali wakifanya vipimo vya COVID-19, Julai 28, 2020.
Wahudumu wa afya wa kituo cha matibabu cha Biomedical Center Kigali wakifanya vipimo vya COVID-19, Julai 28, 2020. AP
Matangazo ya kibiashara

Rwanda ilizindua kampeni ya chanjo Ijumaa, Machi 5, baada ya kupokea dozi karibu 340,000 kama sehemu ya mpango wa shirika la Afya Duniani (WHO) wa Covax, hasa kutoka kwa maabara ya Astra-Zeneca lakini pia kutoka kwa maabara ya Pfizer.

Kwa juma moja, picha za watu kuchomwa sindano zimekuwa zikirushwa kwenye vyombo vya habari nchini Rwanda. Wahudumu wa afya na wazee ni miongoni mwa kundi la kwanza la watu kupewa chanjo hiyo, halafu wafungwa, wakimbizi, waendesha pikipiki za uchukuzi lakini pia wafanyakazi wa shirika la ndege la RwandAir na vile vile wafanyakazi katika hoteli mbalimbali ambao watahudumia wajumbe wa mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Madola, uliopangwa kufanyika katika mji ,kuu wa Rwanda, Kigali, mnamo mwezi Juni.

Rais wa Rwanda Paul Kagame pia alichomwa sindano, na kuwa rais wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kutangaza chanjo yake.

Rwanda ni nchi ya kwanza barani Afrika kutumia chanjo ya Pfizer-BioNtech ambayo inahitaji kuhifadhiwa kwa joto la chini sana. Miezi michache iliyopita Rwanda ilipokea majokofu maalum kwa kuhifadhi chanjo hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.