Pata taarifa kuu
AFYA-UCHUNGUZI

Asili ya Uviko: China yajiona 'imechafuliwa' kwa shutuma za Marekani

Beijing imepinga vikali leoJumatatu nadharia ambayo sasa inazingatiwa na wizara ya ya Nishati ya Marekani (DoE) kwamba Uviko ilitokana na makosa ya kimaabara nchini China, ikijiona kuwa "imechafuliwa" na tuhuma hizi mpya.

Miaka mitatu baada ya kuzuka kwa janga hili, asili ya virusi ambayo vimeua karibu watu milioni 7 ulimwenguni na kutikisa dunia bado haijajulikana.
Miaka mitatu baada ya kuzuka kwa janga hili, asili ya virusi ambayo vimeua karibu watu milioni 7 ulimwenguni na kutikisa dunia bado haijajulikana. AP - Michael Probst
Matangazo ya kibiashara

"Ni muhimu kuacha kuibua nadharia hii ya uvujaji wa maabara, kuacha kuichafua China na kuacha kuingiza siasa katika utafutaji wa asili ya virusi," amebaini msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning, wakati wa mkutano wa kila siku na waandishi wa habari.

Beijing imejibu mabadiliko ya hivi majuzi ya uchanganuzi katika wizara ya Nishati ya Marekani ambayo sasa itabaki - "kwa kiwango cha chini cha uaminifu" - nafasi ya uvujaji wa maabara nchini China, kutokana na kuamini ripoti mpya kutoka kwa idara ya ujasusi iliyofichuliwa Jumapili na Magazeti la Wall Street Journal na New York Times.

"Wataalam kutoka China na shirika la Afya Duniani, WHO, kwa kuzingatia kutembelea maabara huko Wuhan na kuongea kwa kina na watafiti, wamefikia hitimisho la kweli kwamba chaguo la uvujaji kutoka kwa maabara haliwezekani kabisa," Ning amesema.

Miaka mitatu baada ya kuzuka kwa janga hili, asili ya virusi ambayo vimeua karibu watu milioni 7 ulimwenguni na kutikisa dunia bado haijajulikana.

Mnamo Februari 2021, wataalam kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) na wanasayansi wa China waliamua kwamba "haiwezekani" kufuatilia ajali katika taasisi ya virusi ya China huko Wuhan na kupendelea nadharia ya chanzo asilia cha virusi na maambukizi ya mnayama kwa binadamu.

Ishara kwamba mjadala bado uko wazi nchini Marekani, mashirika manne ya ujasusi ya Marekani yanaamini kwamba Uviko inatokana na chanzo asilia na vyanzo viwili bado havijaamua, kulingana na hakiki ya gazeti la Wall Street.

Katikati ya mwezi Februari, Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, binafsi aliahidi kufanya kilio chini ya uwezo wake ili kupata "jibu" juu ya asili ya Uviko-19, akikanusha vikali ripoti kwamba shirika hilo liliachana na kukamilisha uchunguzi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.