Pata taarifa kuu
CHINA- UVIKO 19

China yafungua mipaka yake kwa wageni wa kimataifa

Nchi ya China hatimaye imefungua mipaka yake kwa wageni wa kimataifa, ikiwa ni mara ya kwanza tangu ilipotangaza makataa ya wasafiri mwezi Machi mwaka 2020 kutokana na maambukizo ya uviko19.

Abiria akiwasili katika uwanja wa ndege wa Hangzhou Xiaoshan nchini China.
Abiria akiwasili katika uwanja wa ndege wa Hangzhou Xiaoshan nchini China. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya China, inamaanisha kuwa wageni wote wanaowasili nchini humo hawatahitajika tena kutengwa kwa siku kadhaa, tangazo linalobadili kabisa sera ya nchi hiyo kuhusu ugonjwa wa virusi vya Korona.

Aidha hatua hii imechukuliwa licha ya utawala wa Beijing, hivi karibuni kurekodi ongezeko la maambukizo ya ugonjwa huo.

Hata hivyo, wasafiri wote watalazimika kuonesha ushahidi wa cheti kuwa hawana maambukizo, wakati huu nchi zaidi ya Ulaya na baadhi barani Afrika, zikiweka makataa kwa wasafiri kutoka China ambapo watalazimika kupima virusi hivyo.

Watu zaidi ya laki 4 wanatarajiwa kusafiri kutoka Hong Kong kwenda bara ikiwemo kwenye miji ya Beijing na Xiamen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.