Pata taarifa kuu

China yarekodi vifo zaidi ya 60,000 vya Uviko tangu kuachana na sera yake ya 'sifuri-Uviko'

Takwimu zilizotolewa na Beijing zinazingatia tu vifo vilivyorekodiwa katika vituo vya matibabu, lakini ni vya kwanza kuchapishwa tangu kuondolewa kwa vizuizi vya afya nchini humo mnamo Desemba 8, 2022.

Muuguzi katika hospitali inayohudumia wagonjwa wazee walio na dalili za Uviko-19 huko Fuyang, mkoa wa Anhui mashariki mwa China, Januari 4, 2023.
Muuguzi katika hospitali inayohudumia wagonjwa wazee walio na dalili za Uviko-19 huko Fuyang, mkoa wa Anhui mashariki mwa China, Januari 4, 2023. © Chinatopix via AP
Matangazo ya kibiashara

Siku mbili tu zilizopita, maafisa wakuu wa China walisema ilikuwa mapema sana kufanya hesabu sahihi ya vifo kutoka kwa nimonia ya virusi. "Ni wakati tu janga linapotangazwa ndipo tunaweza kutoa jibu wazi kuhusu kiwango cha vifo vya ugonjwa huo", amesema Liang Wannian, mtaalam mkuu wa tume ya afya ya kitaifa aliyenukuliwa na Gazeti la China Daily. Leo, mamlaka hii ya afya inachapisha ripoti hii rasmi ya kwanza, kulingana na data iliyotolewa na hospitali.

Watu Milioni 900 walioambukizwa

Watu 60,000 walifariki duniani baada ya kuambukizwa virusi vya Corona nchini China, kati ya Desemba 8, 2022 - siku moja baada ya kuondolewa kwa vizuizi vya afya - na Januari 12, 2023. Ongezeko kubwa ikilinganishwa na takriban vifo 5,000 vya Uviko, vilivyoripotiwa na China tangu kuzuka kwa janga hilo. .

Wengi (90%) walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 65, tume imesema. Karibu watu 54,500 walifanyiwa vipimo na kukutwa na virusi vya Corona. Zaidi ya vifo 5,500 vilitokana na "kushindwa kupumua". Hili ni muhimu kufafanua, kwa sababu mamlaka ilionyesha mwezi uliopita kwamba wagonjwa walio na Uviko-19 pekee wanaofariki kwa kushindwa kupumua ndio watakaojumuishwa katika ripoti rasmi za janga hilo.

Tathmini hii ya kwanza ya tume ya afya ya kitaifa inathibitisha hoja iliyotetewa na serikali kadhaa za majimbo ambayo yanathibitisha kwamba kilele cha maambukizi tayari kimepita. Tangazo ambalo linakuja wakati shirika la Afya Dunaini, WHO, Marekani na nchi zingine zikidai uwazi zaidi kutoka kwa China kwenye ripoti zake mpya za maambukizi na vifo.

Takwimu ambazo zimesalia chini ya makadirio yaliyotolewa na taasisi zingine za utafiti wa afya. Je, wimbi la kwanza la janga nchini China limekwisha? Kulingana na taasisi ya Uingereza ya Airfinity, janga hilo lilipaswa kufikia kilele mnamo Januari 13 na watu milioni 3.5 walioambukizwa na vifo zaidi ya 20,000 kwa siku, kwa hivyo kabla ya Mwaka Mpya wa Lunar ambao unaanguka mwaka huu 2023 mnamo Januari 21.

Marekani nayo, hapo awali, ilikuwa imeitaka Iran kutotekeleza adhabu hiyo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.