Pata taarifa kuu

Uviko nchini China: Jumuiya ya kimataifa yajaribu kujipanga

Kutokana na kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa wa Uviko nchini China, ni msimamo gani unapaswa kupitishwa kwa wasafiri kutoka nchini humo? Nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakutana Jumatano hii mjini Brussels kujaribu kupitisha msimamo wa pamoja na WHO, Shirika la Afya Duniani, limekutana na wanasayansi kadhaa wa China ili kujaribu kujadili kwa uwazi zaidi.

Mgonjwa anahamishiwa Idara ya Huduma za Wagonjwa wa Dharura ya Hospitali ya Langfang katika Mkoa wa Hebei. Idara ya Huduma za Wagonjwa wa Dharura katika miji ya kusini magharibi mwa Beijing zimezidiwa.
Mgonjwa anahamishiwa Idara ya Huduma za Wagonjwa wa Dharura ya Hospitali ya Langfang katika Mkoa wa Hebei. Idara ya Huduma za Wagonjwa wa Dharura katika miji ya kusini magharibi mwa Beijing zimezidiwa. AP
Matangazo ya kibiashara

Ni nini hasa kinatokea nchini China kuhusiana na Uviko? Swali ambalo limesalia bila jibu kwani viongozi wa China wanakaa kimya juu ya uzito wa janga hilo. Beijing, kwa mfano, ilithibitisha vifo vipya vitano siku ya Jumanne Januari 3 wakati wataalam wa kutoka nchi za Magharibi wanakadiria kuwa maelfu kadhaa wanafariki dunia kwa siku kutokana na ugonjwa huu hatari wa Uviko.

WHO, ambayo imebadilisha kwa kiasi kikubwa kauli yake katika miezi ya hivi karibuni na Beijing, imeandaa mkutano na wataalam kutoka China. Bado hakuna maelezo yaliyovuja kuhusu mkutano huu, lakini ni vigumu kuona jinsi shirika la Umoja wa Mataifa litafaulu kuwashawishi wajumbe kutoka Beijing, anaripoti mwandishi wetu huko Geneva, Jérémie Lanche. Kwa miezi kadhaa shirika hilo limekuwa likiuliza China kutoa data yake juu ya wagonjwa hospitalini, wagonjwa mahututi, vifo na idadi ya wagonjwa walioambukizwa virusi hivyo, Bila mafanikio, hadi sasa.

WHO huwa haikosoi nchi wanachama wake. Inaongeza umakini wake maradufu linapokuja suala la kutoa maoni juu ya hatua za China. Lakini mtu hawezi kujizuia kuona kero ya maafisa wa WHO. Kuona shirika hilo likilaumu hadharani ukosefu wa uwazi wa Beijing na hata kusema kwamba linaelewa vikwazo vilivyowekwa na nchi kadhaa kwa wasafiri kutoka China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.