Pata taarifa kuu
UVIKO-AFYA

UVIKO: Wachina wapokea kwa shangwe uamuzi wa serikali kuondoa karantini

Watu nchini China, wamepokea kwa furaha, tangazo la serikali kuondoa sharti la kuwekwa karatini kwa wageno wote wanaowasili nchini humo, lililowekwa miaka mitatu iliyopita, ili kupambana na mamabukizi ya UVIKO 19.

Wanawake wawili wakivaa mavazi maalumu ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Corona karibu na soko la Xinfadi, ambapo mlipuko mpya wa Corona umeanzia, Beijing Juni 13, 2020.
Wanawake wawili wakivaa mavazi maalumu ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Corona karibu na soko la Xinfadi, ambapo mlipuko mpya wa Corona umeanzia, Beijing Juni 13, 2020. GREG BAKER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia Januari tarehe 8 mwaka ujao, ikiwa na maana kuwa abiria wote wanaowasili nchini humo, hawatawekwa karatini.

Tangazo hili la Beijing, linakuja pia baada ya kuwepo kwa maandamano ya wik kadhaa zilizopinga kupinga harakati za serikali kuendelea kuweka vikwazo vya kupambana na maambukizi hayo yanaonekana kuongeza tena katika siku za hivi karibuni.

Tangu mwezi Machi mwaka 2020, China iliweka vikwazo dhidi ya abiria wote waliokuwa wanawasili nchini humo na kuwataka kukaa karantini, lakini tangazo hili, limefanya watu nchini humo kupanga safari kwenda kuwatembelea ndugu zao.

China inakuwa nchi ya mwisho yenye uchumi mkubwa duniani, kufungua nchi yake, licha ya ripoti kuwa wiki iliyopita pekee, watu zaidi ya Elfu nne waliambukizwa wengi wao wazee, baadhi yao wakipoteza maisha.

Licha ya kondolewa kwa sharti la kuwekwa karantini,  abiria wanaowasili nchini humo watahitajika, kupimwa ili kubaini kuwa hawa maambukizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.