Pata taarifa kuu

China yasitisha kutangaza takwimu za kila siku za UVIKO-19

Kwa kuzidiwa na wimbi ambalo halijawahi kushuhudiwa la UVIKO, mamlaka ya afya nchini China imetangaza kusitishwa kwa uchapishaji wa tathmini yao ya kila siku ya ugonjwa huo. Takwimu hizi rasmi zimekuwa na utata tangu kuachwa kwa hatua za kudhibiti na kuzuia nimonia ya virusi wiki tatu zilizopita.

Mamlaka ya afya ya China imetangaza kusitishwa kwa uchapishaji wa ripoti yao ya kila siku ya UVIKO. Hapa, watu waliofunika nyuso zao wakienda kazini asubuhi, huko Beijing, mnamo Desemba 20, 2022.
Mamlaka ya afya ya China imetangaza kusitishwa kwa uchapishaji wa ripoti yao ya kila siku ya UVIKO. Hapa, watu waliofunika nyuso zao wakienda kazini asubuhi, huko Beijing, mnamo Desemba 20, 2022. AP - Andy Wong
Matangazo ya kibiashara

Licha ya ongezeko la rekodi la visa vya maambukizi kote nchini, hakuna kifo kilichoripotiwa rasmi na mamlaka katika siku tano zilizopita.

Tume ya kitaifa ya Afya imetangaza kwanza kumalizika kwa uzingatiaji wa watu wasio na dalili katika tathmini zake, kisha kufafanua upya vigezo vya vifo vinavyosababishwa na UVIKO. Kufikia Desemba 25, taasisi hiyo imesutisha uchapishaji wa takwimu za kila siku za ugonjwa huu. Takwimu hizi zinatiliwa shaka, hasa zinapolinganishwa na zile zinazotolewa na serikali nchini humo.

Jumapili hii, Desemba 25, serikali ya Zhejiang imetoa tahadhari. Mkoa huu ulioko mashariki mwa China, ambao una wakazi wengi kama Italia au Afrika Kusini, unarekodi maambukizi mapya milioni 1 kwa siku, idadi ambayo inatarajiwa kuongezeka maradufu hivi karibuni. Kilele cha maambukizo kinakadiriwa kuja karibu na Mwaka Mpya wa Lunar, mwishoni mwa mwezi wa Januari kulingana na mamlaka ya mkoa, wakati makumi ya mamilioni ya Wachina watasafiri kwa likizo ya Tamasha la Spring au mwezi wa kwanza wa mwandamo wa Kichina ambao hujulikana kama "Mwaka Mpya wa Kichina" "Mwaka Mpya wa Lunar" au "Mwaka Mpya".

Kinga ya mifugo

"China inaingia katika wiki hatari zaidi za janga hili," imesema barua kutoka kwa taasisi ya Capital Economics iliyonukuliwa na shirika la habari la Reuters. Mamlaka hazifanyi juhudi zozote sasa kupunguza kuenea kwa maambukizi.

Baada ya kuzungumza juu ya wimbi la kwanza la UVIKO, vyombo vya habari vya serikali sasa vinazungumza juu ya "wimbi la mwisho la UVIKO". Shirika la Afya Duniani linasema halijapokea data yoyote juu ya kulazwa hospitalini kuhusishwa na nimonia ya virusi nchini China tangu serikali ya China kulegeza vikwazo vya afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.