China yarekodi visa vingi vya maambukizi ya virusi vya Uviko 19
China imeandikisha idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Uviko 19 tangu kuzuka tena kwa maambukizi hayo mwezi Aprili, licha ya masharti mapya ya kukabiliana na janga hilo.
Imechapishwa:
Ripoti zinasema kwa muda was aa 24 zilizopita, watu 31,527 wameambukizwa. Mara ya mwisho kwa nchi hiyo kushuhudia idadi kubwa ya maambukizi kwa siku moja ilikuwa ni mwezi Aprili, ambapo watu Elfu 28 waliambukizwa.
Maambukizi haya mapya yameanza kushuhudiwa katika jiji kuu Beijing na mji wa kibiashara wa Guangzhou.
Hata hivyo, watalaam wa afya wanasema idadi hii ni ndogo kwa taifa hilo lenye watu Bilioni 1.4 na tangu kuzuka kwa ugonjwa huu ulioanzia nchini himo miaka miwili iliyopita, watu 5,200 ndio walippoteza maisha.
China imekuja na sera ya kuhakikisha kuwa, kuna sifuri ya maambukizi ya virusi hivyo, hatua ambayo imesaidia kuokoa maisha ya watu, lakini imetatiza uchumi wa nchi hiyo ya bara Asia.