Pata taarifa kuu

COVID-19: China yatoa wito kwa wakaazi wake kuhifadhi chakula

China ambayo inakabiliwa na kuzuka tena kwa janga la COVID, inataka kuzuia uhaba mkubwa wa chakula na bidhaa mahitajio, ambao ulikuwa umeikumba nchi hiyo mnamo mwaka 2020.

Takriban watu milioni 6 wamepigwa marufuku ya kutembea, ikiwa ni pamoja na katika jiji kubwa la Lanzhou, kilomita 1,700 magharibi mwa Beijing.
Takriban watu milioni 6 wamepigwa marufuku ya kutembea, ikiwa ni pamoja na katika jiji kubwa la Lanzhou, kilomita 1,700 magharibi mwa Beijing. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Katika tangazo lililochapishwa kwenye tovuti yake jioni ya Jumatatu Novemba 1, Wizara ya Biashara ya China imetoa wito kwa raia wa China  "kuhifadhi kiasi fulani cha mahitaji ya kimsingi ili kukidhi mahitaji ya kila siku na dharura." Hata hivyo, ombi hili kutoka kwa onyo hili linatolewa au kwa sababu gani.

Ushauri wa Wizara ya Biashara unakuja huku kukiwa na hofu ya kuzuka tena kwa janaga la COVID-19. Kuzuka kwa janga la COVID-19 mnamo mwaka wa 2020, katika kilele cha mzozo wa Covid, mfumo wa usambazaji wa China ulitatizwa sana, na kusababisha uhaba mwingi wa chakula na bidhaa zingine mahitajio.

Wakati inakaribia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi huko Beijing mwezi Februari mwakani, serikali ya China ina hofu ya kuzuka kwa janga jipya na imechukua hatua kali katika wiki za hivi karibuni kufuatia kuonekana kwa milipuko ya mara kwa mara ya COVID-19 kaskazini mwa nchi.

Takriban watu milioni 6 wamepigwa marufuku ya kutembea, ikiwa ni pamoja na katika jiji kubwa la Lanzhou, kilomita 1,700 magharibi mwa Beijing. Hata hivyo, idadi ya kesi zilizothibitishwa bado ni ndogo sana ikilinganishwa na idadi zilizorekodiwa ulimwenguni. Kesi 71 pekee za maambukizi zimetangazwa Jumanne hii kwa kipindi cha saa 24 zilizopita, baada ya kesi 92 Jumatatu, hesabu kubwa zaidi ya kitaifa tangu katikati ya mwezi Septemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.