Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Biden ashutumu China kwa kuficha 'habari muhimu' juu ya chimbuko la Covid-19

Rais wa Marekani Joe Biden ameituhumu China kwa kupotosha "habari muhimu juu ya chimbuko la janga la Covid-19" baada ya kuchapishwa kwa muhtasari wa ripoti ya uchunguzi wa ujasusi wa Marekani, ikionyesha kuwa haiwezi kuamua juu ya suala hilo.

Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

"Ripoti ya idara ya ujasusi ya Marekani inaonyesha kuwa Marekani imeazimia kuchukua njia mbaya ya kutumia kisiasa," ubalozi wa China nchini Marekani umebaini leo Jumamosi katika taarifa. "Ripoti ya idara ya ujasusi inaonekana kuwa ni kama shutma zisizo kuwa na msingi dhidi ya China, na kuifanya China ianukie pua wao wanufaike."

Ripoti hii ambayo imzewekwa kama siri kuu iliwasilishwa wiki hii kwa rais wa Marekani, ambaye alikuwa ameipa siku 90 idara ya ujasusi "kuongeza juhudi zao" kuelezea chimbuko la janga hilo.

Kulingana na muhtasari uliotolewa Ijumaa, ujasusi uhitimisha kuwa SARS-CoV-2, jina la kisayansi la virusi, haikutengenezwa "kama silaha ya kibaolojia".

Lakini bado wamegawanyika kati ya nadharia ya kesi ya kwanza iliyosababishwa na mlipuko wa asili kwa mnyama aliyeambukizwa, au kutokana na ajali ya maabara.

"Habari muhimu juu ya chimbuko la janga hilo iko nchini China, na bado tangu mwanzo, maafisa wa serikali nchini China wamekuwa wakifanya kazi kuzuia wachunguzi wa kimataifa na watendaji wa afya ya umma kuingia nchini humo," rais wa Marekani ameshtumu katika taarifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.