Pata taarifa kuu

Covid: Beijing kufawanyia vipimo wakaazi wake milioni 2

Nchini China, aina mpya ya kirusi cha Omicron kimebisha hodi wiki mbili zilizopita na kwa sasa, sio mlipuko ambao umeshuhudiwa mahali pengine duniani, kwani nchi hii inaendelea kutumia sera kali kwa kesi ndogo zaidi.

Ili kuzuia kuenea kwa Covid, Beijing imetangaza kwamba wenyeji milioni mbili watafanuiwa vipimo.
Ili kuzuia kuenea kwa Covid, Beijing imetangaza kwamba wenyeji milioni mbili watafanuiwa vipimo. © Andy Wong/AP
Matangazo ya kibiashara

Lakini wiki mbili kabla ya kuanzishwa kwa mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi huko Beijing, mji mkuu wa China umerekodi karibu kesi thelathini katika siku chache. Kwa hivyo, ili kuzuia kuenea kwa kirusi hiki, Beijing imetangaza Jumamosi hii, Januari 23, kwamba wakazi milioni mbili watafanyiwa vipimo.

Kwa wiki chache tayari, Beijing imekuwa chini ya shinikizo: kabla ya kuandaa mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi, jiji hilo hasa halitaki kuona kesi zozote za Covid zikienea.

Lakini kutokana na kirusi kipya cha Omicron kinachoambukia kwa haraka, ilikuwa ni suala tu la muda: wiki moja iliyopita, kesi ya kwanza iligunduliwa na tangu wakati huo kesi kama hizo huripotiwa kwa kiwango kdogo polepole.

Mkakati ulioboreshwa vyema

Leo, wilaya iliyo kusini mwa jiji ambapo mlipuko uligunduliwa imeamua kuwafanyia vipimo wakaazi wake milioni mbili. Huu ni mkakati wa kawaida nchini China, kufanyia vipimo idadi kubwa ya watu. Magharibi mwa Beijing, wakaazi milioni 13 wa jiji la Xi'an wanakaribia kutoka kwa mwezi mmoja wa kuwekwa karantini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.