Pata taarifa kuu

China yashuhudia ongezeko la visa vya Covid-19

Watu zaidi ya Milioni 30 wamewekewa masharti ya kutotembea nchini China siku ya Jumanne, kufuatia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Covid-19 kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili. 

Nchini China, wahudumu wa afya wakiwa wamevalia mavazi ya kujikinga dhidi ya Covid-19, kufuatia kuzuka kwa Covid-19 huko Changchun, katika mkoa wa Jilin mnamo Machi 14, 2022.
Nchini China, wahudumu wa afya wakiwa wamevalia mavazi ya kujikinga dhidi ya Covid-19, kufuatia kuzuka kwa Covid-19 huko Changchun, katika mkoa wa Jilin mnamo Machi 14, 2022. VIA REUTERS - CHINA DAILY
Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja baada ya China siku ya Jumanne kuripoti visa vipya 5,280 vya Corona, vya kirusi cha omicron. 

Miji 13 nchini humo imefungwa; kuzuia maambukizi zaidi baada ya kuriptiwa kuwa, tangu mwezi Machi, watu Elfu 15 walikuwa wameambukizwa  corona. 

Wakati hatua hii ikichukuliwa, Wizara ya afya nchini humo, imewataka watu wenye zaidi ya miaka 60 kupata chanjo na kuongeza dozi ya tatu ili kupambana na maambukizi hayo. 

Mbali na hilo, safari za ndani kati ya miji ya Beijing na Shanghai, zimefutwa na safari za ndege 100 za Kiamtaifa ambazo zilikuwa ziende mjini Shanghai zitakwenda katika miji mingine kuanzia wiki ijayo hadi Mei mosi. 

Kirusi cha Corona duniani, kilianzia mji wa Wuhan mapema mwaka 2020 na kusambaa kote duniani, lakini kwa sasa maisha yamerejea kama kawaida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.