Pata taarifa kuu

Corona yazidi kutishia Beijing, vyumba vya dharura vyazidiwa

Idadi ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona inaendelea kuongezeka katika mji mkuu wa China, Beijing. Kwa sasa vyumba vya dharura katika hospitali mbalimbali vimezidiwa na idadi ya wagonjwa inaendelea kuongezeka.

Wachina hawa wakiandamana na ndugu zao wagonjwa kwenye chumba cha dharura katika hospitali ya Bahzou, kaskazini mwa China mnamo Desemba 22, 2022.
Wachina hawa wakiandamana na ndugu zao wagonjwa kwenye chumba cha dharura katika hospitali ya Bahzou, kaskazini mwa China mnamo Desemba 22, 2022. © Dake Kang / AP
Matangazo ya kibiashara

Kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona, ni tishio kubwa kwa mamlaka ya China, wakati ugonjwa huo ulikuwa umedhibitiwa nchini humo.

Kwa kuzingatia ukubwa wa wimbi la UVIKO-19 huko Beijing, vyumba vya dharura vimejaa. Mamlaka zimeainisha tena ugonjwa huo, na vigezo vinavyofafanua vifo vinavyohusishwa na nimonia ya virusi. "Baba yangu ana umri wa miaka 93, anaugua nimonia ya kawaida kulingana na madaktari. Lakini, amepimwa na amepatikana na virusi vya Corona, kama wagonjwa wengi katika huduma hii ambao wote wameambukizwa na virusi hivyo, "anaongeza mkaazi huyo wa Beijing.

'Nimonia ya kawaida', mshtuko wa moyo… Jumapili Desemba 25, Tume ya kitaifa ya Afya ilihitimisha uchapishaji wa ripoti zake za kila siku kuhusu janga hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.