Pata taarifa kuu

Michelle Bachelet: Watu hawapaswi kuchanjwa kwa lazima

Wajibu wa chanjo lazima kila wakati uheshimu haki za binadamu na chanjo ya kulazimishwa haikubaliki kamwe, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu ameonya Jumatano. Pamoja na aina ya tano ya kirusi cha Corona, mjadala juu ya wajibu wa chanjo unafanywa kuwa muhimu zaidi.

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Michelle Bachelet.
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Michelle Bachelet. Fabrice COFFRINI AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati mlipuko wa 5 wa maambukizi ya Covid ukienea kote Ulaya, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amekumbusha wakati wa semina juu ya ufikiaji wa huduma ya afya kwamba jukumu la chanjo linapaswa "kuendana na kanuni za uhalali, umuhimu, uwiano na kutobagua".

"Katika hali yoyote ile watu wasipewe chanjo ya lazima, ingawa kukataa kwa mtu kutii wajibu wa chanjo kunaweza kuwa na matokeo ya kisheria kama vile kutozwa faini inayofaa," amesema Michelle Bachelet katika ujumbe wa video.

Austria, kwa mfano, imeamua kufanya chanjo kuwa ya lazima kwa kila mtu kuanzia tarehe 1 Februari. Ujerumani pia inazingatia suluhisho hili chini ya uongozi wa Kansela mpya Olaf Scholz. Hatua za kiafya zilizochukuliwa kutokana na kiwango cha chanjo kinachokadiriwa kuwa si cha juu vya kutosha na mamlaka.

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen ametoa wito wa kufunguliwa kwa mjadala juu ya mada hiyo na Shirika la Afya Dunia, linasisitiza juu ya dhana ya "suluhisho la mwisho kabisa" kwa sababu ya athari za maadili na vitendo. Kwa upande wa Michelle Bachelet, anasema "wajibu wa chanjo inapaswa kutumika tu wakati inahitajika kufikia malengo muhimu ya kiafya na inapaswa kuzingatiwa tu wakati hatua zisizoingiliana kama vile kuvaa barakoa na watu kutokaribiana, zimeonyesha kuwa zimeshindwa kufikia malengo haya. ”.

Pia amekumbusha udharura wa kufanya chanjo upatikane kwa wote ili kuheshimu kanuni ya usawa na kutobagua. Kwa upande mwingine, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu anaona kwamba itakuwa halali kuzuia baadhi ya haki na uhuru wa wale wanaokataa kutii wajibu wa chanjo (kupata nafasi katika shule, kupewa nafasi ya kuhudumiwa hospitalini au katika maeneo mengine ya umma).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.