Pata taarifa kuu

Dunia yaonywa kuhusiana na afya ya binadamu kufuatia kirusi cha Omicron

Mgunduzi wa chanjo aina ya Oxford/AstraZeneca, ya kupambana na janga la Covid-19, Sarah Gilbert, anaonya juu ya uwezekano kuhusu janga lijalo la afya huenda likawa baya zaidi na hivyo dunia inapaswa kujiandaa vya kutosha.

Wito huu unakuja, wakati huu dunia inapokabiliana na aina mpya ya kirusi kilichopewa jina la Omicron, ambacho kinaendelea kusambaa kwa kasi hasa nchini Afrika Kusini ilikogunduliwa na mataifa mengine kama Uingereza.
Wito huu unakuja, wakati huu dunia inapokabiliana na aina mpya ya kirusi kilichopewa jina la Omicron, ambacho kinaendelea kusambaa kwa kasi hasa nchini Afrika Kusini ilikogunduliwa na mataifa mengine kama Uingereza. Frederic J. BROWN AFP
Matangazo ya kibiashara

Mtaaam huyo amesema, dunia inapaswa kujifunza na kilichotokea baada ya kuzuka kwa janga la Covid-19 na kutaka dunia kuanza maandalizi mapema, akionya kuwa haitakuwa mara ya mwisho kwa kirusi kutishia maisha ya watu duniani.

Wito huu unakuja, wakati huu dunia inapokabiliana na aina mpya ya kirusi kilichopewa jina la Omicron, ambacho kinaendelea kusambaa kwa kasi hasa nchini Afrika Kusini ilikogunduliwa na mataifa mengine kama Uingereza.

Watalaam wanaonya kuwa, huenda kirusi hiki cha Omicron kikasambaa kwa kasi nchini Uingereza, wakati huu kukiwa na hofu kuwa mpaka sasa watu zaidi ya Elfu moja wameambukizwa kirusi hicho kipya.

Wanasayansi wanaochunguza kirusi hiki kipya, wana hofu kuwa huenda kikasambaa kwa kasi kwa kile wanachosema kirushi hicho kinabadilika mara kwa mara.

Hata hivyo, watalaam hao wanasema itachukua muda kubaini athari ambazo huenda zikatokea duniani, kufuatia kirusi hiki kipya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.