Pata taarifa kuu

Omicron: UN, AU walaani "ubaguzi" unaoathiri baadhi ya nchi za kusini mwa Afrika

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (AU) kwa pamoja wamelaani "ubaguzi" ambao baadhi ya nchi za kusini mwa Afrika zimekuwa zikikabiliwa nao tangu kugunduliwa kwa kirusi kipya cha Omicron nchini Afrika Kusini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa Afrika "Afrika "imehukumiwa" mara mbili katika janga hili la Covid-19.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa Afrika "Afrika "imehukumiwa" mara mbili katika janga hili la Covid-19. Kenzo TRIBOUILLARD POOL/AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa tume ya AU alikuwa katika Umoja wa Mataifa, ambapo alikutana na katibu mkuu kwa mkutano wao wa kila mwaka. Na ni habari iliyochukua nafasi ya kwanza kuliko tafakari zao za kawaida za kidiplomasia.

Antonio Guterres na Moussa Faki Mahamat wamejitokeza pamoja kwa kuelezea hasira yao, kutokana na hatua ya kufungwa kwa mipaka iliyotangazwa na nchi mbalimbali duniani. Katibu Mkuu wa wa Umoja wa Mataifa alisisitiza kuwa Afrika "imehukumiwa" mara mbili katika janga hili, kwa kukosa kupata chanjo za kutosha kwanza, na kwa sasa kukwama katika kufufua uchumi wake. alitoa maneno makali: “Tuna vifaa vya kusafiri kwa usalama. Basi tuvitumie vyombo hivi ili kuepukana na hali hii...kama mtaniruhusu niseme hivyo...ubaguzi wa kusafiri! "

Udhalimu

Udhalimu huu, ubaguzi huu usio na msingi, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Moussa Faki Mahamat pia amezishambulia nchi hizo kwa maeneo makali. Hasa wakati hatua hizi zinachukuliwa wakati huu wa sherehe za majira ya joto na mwisho wa mwaka, sawa na kurejesha shughuli za utalii na kufufua uchumi. "Ilibainika kuwa virusi hivi vilikuwepo katika nchi moja au mbili za Ulaya muda mrefu kabla ya ugunduzi uliofanywa na Afrika Kusini," mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika amesema.

Vizuizi visivyo na msingi

Moussa Faki Mahamat alieleza kuwa shirika lake, Umoja wa Mataifa, WHO na mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Afrika, CDC, wanafanya kinachowezekana kuyafanya mataifa haya kuelewa kwamba, kisayansi vikwazo hivi havina uhalali, wakitumaini kwamba vitaondolewa hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.