Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Algeria yashindwa kuvunja rekodi ya Ubelgiji, yakubali kipigo cha bao 2-1, Mexico Brazil hakuna mbabe

Michuano ya kombe la dunia imeendelea tena siku ya Jumanne kwa wawakilishi wengine wa Afrika kwenye michuano hii, timu ya taifa ya Algeria kushindwa kuliwakilisha vema bara hili, baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Ubelgiji. 

Mchezaji wa Algeria, Sofiane Feghouli akiifungia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Ubelgiji
Mchezaji wa Algeria, Sofiane Feghouli akiifungia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Ubelgiji REUTERS/Dominic Ebenbichler
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mchezo huo ambao Algeria walicheza kwa kasi sana kwenye kipindi cha kwanza, ilishuhudiwa timu hiyo ikiwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 25 kwa njia ya penati, penati ambayo iliwekwa kimiani na mchezajiSofiane Feghouli.

Bao hili lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinapotamatika, ambapo timu hizi zilienda mapumziko huku Algeria ikiwa inaongoza kwa bao moja mbele ya Ubelgiji ambapo kutokana na kiwango kilichokuwa kimeonesha na Algeria kila mtu aliamini kuwa Algeria wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zote mbili zikifanya mashambulizi ya hatari ambayo kama si juhudi za mabeki na makipa wao basi kwenye mechi ya jana yangeshuhudiwa mabo mengi kwenye mechi moja.

Ubelgiji ambayo haina historia ya kufungwa na timu yoyote kutoka barani Afrika kwenye michuano ya kombe la dunia, iliendelea kuweka rekodi yake baada ya kusawazisha bao kupitia kwa kiungo Maroun Fellaini aliyeingia kipindi cha pili, bao hili lilipatka katika dakika ya 70 akipokea basi kutoka kwa De Bruyne.

Ubelgiji walijipatia bao la ushindi katika dakika ya 80 ya mchezo lililofungwa na Dries Martens baada ya kuunganisha vema pasi aliyopewa na kiungo mshambuliaji Eden Hazard.

Mara baada ya bao hilo Algeria walijaribu kutafuta bao la kuswazisha bila mafanikio ambapo mpaka mwamuzi wa mchezi huu anapuliza filimbi ya mwisho, Ubelgiji walitoka kifua mbele kwa mabao 2-1.

Mechi nyingine ya kundi H ilikuwa ni ilt kati ya timu ya taifa ya Urusi waliokuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Jamhuri ya watu wa Korea, kwenye mchezo ambao ulikuwa wa kukata na shoka kwa muda wote wa mchezo.

Timu ya Korea Kusini ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 68 ya mchezo, bao lililowekwa kimiani na mchezaji, Keun-Ho Lee ambaye aliunganisha vema mpira wa pasi aliopewa na mchezaji Kook-Young Han.

Bao hili liliwapa nguvu vijana wa Korea Kusini ambao walizidisha mashambulizi kwenye lango la Urusi na kumpa wakati mgumu mlinda mlango wa Urusi, Igor Akinfeev ambaye mara nyingi alijikuta akifanya makosa ya kizembe kwa kupoteza mipira ya mbali iliyokuwa ikipigwa kuelekea langoni mwake.

Urusi walikuja juu na katika dakika ya 74 ya mchezo walifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Alexander Kerzhakov aliyeingia saa chache kuchukua nafasi ya Yury Zhirkov.

Mpaka mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho kumaliza mchezo huu, timu ya taifa ya Urusi na Korea Kusini zilitoka sare ya bao 1-1.

Mchezo mwingine ulikuwa ni ule wa kundi A ambapo timu ya taifa ya Mexico ilikuwa na kibarua dhidi ya wenyeji wa michuano ya mwaka huu timu ya taifa ya Brazil kwenye mchezo ambao ulishuhudia timu hizi sikipata sare tasa.

Timu zote mbili ziliingia uwanjani huku kila mmoja akitaka kuvunja rekodi ya mwenzake, lakini washambuliaji wake hawakuweza kuzifumania nyavu kwa wakati licha ya kupata nafasi nyingi ambazo wangeweza kuzitumia kubadili matokeo.

Shujaa wa mchezo huo alikuwa ni mlinda mlango wa Mexico Guillermo Ochio ambaye aliokoa michomo mingi iliyokuwa ikielekezwa langoni mwake na washambuliaji wa Brazil walioongozwa na kinda Neymar pamoja na Fred.

Kwa matokeo haya sasa, Brazil wanaongoza kundi A wakiwa na alama 4 wakifuatiwa na Mexico wenye alama 4 huku Croatia na Cameroon zenyewe zikiwa hazina alama yoyote.

Leo kutakuwa na mechi kadhaa ambazo zitapigwa, kwenye kundi A wawakilishi wa Afrika simba wasiofugika timu ya taifa ya Cameroon watatupa karata yao ya pili dhidi ya timu ya taifa ya Croatia kwenye mchezo ambao ni muhimu kwa timu zote mbili kwakuwa zinahitaji ushindi ili walau kuweza kufufua matumaini ya kusonga mbele.

Mechi nyingine zitakuwa ni zile za kundi B ambapo timu ya taifa ya Australia itakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi ambayo inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata ushindi kwenye mchezo wake wa awali dhidi ya Uhispania.

Uhispania wenyewe wataingia kwenye mchezo huu wa kundi B wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa awali kwa kichapo cha mabao 5 kwa 1 dhidi ya Uhispania, inapambana na timu ya taifa ya Chile ambayo yenyewe ilianza kwa ushindi michuano ya mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.