Canada yatishia kujiondoa katika mkutano wa G8 utakaofanyikia Urusi
Waziri mkuu wa Canada Stephen Harper ametishia kujiunga na serikali ya Washington kuahirisha mkutano wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda duniani G8 mjini Sochi Urusi, ikiwa nchi hiyo itaingilia uhuru wa Ukraine.
Imechapishwa:
Uamuzi wa bunge la Urusi kuidhinisha raisi wa taifa hilo kutuma majeshi katika nchi jirani ya Ukraine umesababisha kauli mbalimbali kutoka kwa jamii za kimataifa.
Waziri Harper amelaani hatua ya urusi kuingilia kijeshi nchini Ukraine kwa kuona kuwa uamuzi huo ni kuingilia uhuru wa Ukraine lakini pia urusi inakiuka sheria ya kimataifa inayohusu majukumu ya taifa binafsi.
Awali raisi wa Marekani Barack Obama alisema atasimama pamoja na jumuiya ya kimataifa katika kuhakikisha kwamba kutakuwa na gharama kwa uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na kuuondoa mkutano wa G8 mjini Sochi mwezi Juni mwaka huu.