Pata taarifa kuu
SHERIA-USALAMA

Beijing yashutumu 'baadhi ya nchi' kwa 'kukashifu' sheria mpya ya usalama wa kitaifa

China imekashifu tabia ya "baadhi ya nchi" ambazo "zinakashifu" sheria mpya ya usalama wa kitaifa huko Hong Kong, ikitoa kifungo cha maisha kwa makosa kama vile uhaini na uasi. 

Wabunge wanapigia kura Kifungu cha 23 cha Sheria ya Usalama wa Kitaifa, huko Hong Kong mnamo Machi 19, 2024. Bunge la Hong Kong lilipitisha kwa kauli moja sheria mpya ya usalama wa kitaifa mnamo Machi 19, ikianzisha adhabu kama vile kifungo cha maisha jela kwa uhalifu unaohusiana na uhaini na uasi, na kifungo cha hadi miaka 20 jela kwa wizi wa siri za serikali.
Wabunge wanapigia kura Kifungu cha 23 cha Sheria ya Usalama wa Kitaifa, huko Hong Kong mnamo Machi 19, 2024. Bunge la Hong Kong lilipitisha kwa kauli moja sheria mpya ya usalama wa kitaifa mnamo Machi 19, ikianzisha adhabu kama vile kifungo cha maisha jela kwa uhalifu unaohusiana na uhaini na uasi, na kifungo cha hadi miaka 20 jela kwa wizi wa siri za serikali. AFP - PETER PARKS
Matangazo ya kibiashara

"China inaelezea kutoridhika kwake na upinzani mkali kwa baadhi ya nchi na mashirika ambayo yanadharau na kukashifu sheria ya usalama wa kitaifa huko Hong Kong," msemaji wa diplomasia ya China, Lin Jian, amevambia vyombo vya habari", linaripoti shirika la habari la AFP.

Siku ya Jumanne Bunge la Hong Kong, eneo la China linalojitawala, lilipiga kura kwa kauli moja kwa sheria mpya ya usalama wa kitaifa ambayo inaleta wasiwasi katika nchi za Magharibi. Rasimu iliyopitishwa na Baraza la Bunge linakamilisha sheria ya usalama wa kitaifa iliyowekwa na Beijing mnamo mwaka 2020 baada ya maandamano makubwa ya mwaka ya mwaka 2019 ya kuunga mkono demokrasia huko Hong Kong.

Makundi matano ya ziada ya makosa

Sheria hiyo mpya imeorodhesha aina tano za makosa pamoja na yale yaliyoadhibiwa na nakala ya 2020: uhaini, uasi, ujasusi na wizi wa siri za serikali, hujuma zinazohatarisha usalama wa taifa, uchochezi na "kushirikiana na nchi za kigeni kwa kuhujumu usalama wa taifa".

Marekani, Uingereza, Umoja wa Ulaya pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara na watetezi wa haki za binadamu wana wasiwasi kuhusu sheria ambayo itazuia zaidi uhuru huko Hong Kong.

"Usalama ni sharti la maendeleo, na utawala wa sheria ndio msingi wa ustawi," msemaji wa diplomasia ya China Lin Jian amesema. "Shambulio lolote na kashfa dhidi ya sheria ya usalama wa taifa (...) bila shaka vitashindwa," aamebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.