Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Hong Kong: Watu 47 wanaounga mkono demokrasia wahukumiwa kwa kuhatarisha usalama wa taifa

Kesi ya viongozi 47 wa upinzani, wakiwemo viongozi wengi wa kisiasa huko Hong Kong, ilianza Jumatatu, Februari 6. Wanaume na wanawake hawa wanashtakiwa kwa uchochezi kufuatia ushiriki wao katika uchaguzi wa Julai 2020 na wakipatikana na hatia, wanakabiliwa na vifungo vizito vya hadi maisha jela.

Maandamano ya kuunga mkono demokrasia huko Hong Kong, tarehe 8 Desemba 2019.
Maandamano ya kuunga mkono demokrasia huko Hong Kong, tarehe 8 Desemba 2019. REUTERS / Danish Siddiqui
Matangazo ya kibiashara

Kati ya washtakiwa 47 waliopandishwa kizimbani, angalau nusu ni watu wanaojulikana na hata vinara wa siasa za Hong Kong, viongozi wa vyama na wabunge wakongwe. Wengine, kinyume chake, ni vijana na watu wapya katika siasa za Hong Kong, wanawakilisha upinzani mpya.

Mstakabali unaoharibiwa na sheria ya usalama wa taifa. Hakuna tena upinzani wowote unaounga demokrasia huko Hong Kong na ni kupitia kesi hii ambapo mamlaka itajaribu kuwaondoa katika maisha ya kisiasa wale walioifanya kuwepo.

'Mateso ya kisiasa'

"Nadhani kesi hii ni mateso ya kisiasa na ni mzaha katika kila maana ya neno. Kwa sababu hakimu yeyote mwenye uadilifu wowote, mfumo wowote wa kisheria unaozingatia sheria za kawaida na kuheshimu haki za binadamu ungetupilia mbali kesi hii miaka miwili iliyopita,” amesema wakili Dennis Kwok, mwanachama wa zamani wa Chama cha Wananchi, ambaye yuko uhamishoni Marekani.

Kati ya watu 47 walioshtakiwa, 34 wamewekwa gerezani kwa karibu miaka miwili, kama hatua ya kuzuia wasitoroke. Kumi na sita waliamua kukiri makosa, kwa matumaini ya kupunguziwa vifungo vyao. Na watatu walikubali kuwa mashahidi wa upande wa mashtaka. Kesi hiyo inatarajiwa kudumu hadi msimu wa joto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.