Pata taarifa kuu

Kituo cha habari kinachounga mkono demokrasia chavamiwa na polisi Hong Kong

Shambulio lingine dhidi ya uhuru wa wanahabari limetokea Jumatano hii, Desemba 29 huko Hong Kong. Leo asubuhi, mapema alfajiri, ofisi za kituo cha habari cha Stand News, mojawapo ya vyombo vya habari huru vya mwisho katika kanda maalum ya utawala, kimevamiwa na polisi. Sita kati ya viongozi wa kituo hiki au viongozi wake wa zamani wamekamatwa wakiwa majumbani mwao.

Maafisa wa polisi wakipiga kambi mbele ya jengo la ofisi ya Stand News huko Hong Kong, Jumatano hii, Desemba 29.
Maafisa wa polisi wakipiga kambi mbele ya jengo la ofisi ya Stand News huko Hong Kong, Jumatano hii, Desemba 29. AP - Vincent Yu
Matangazo ya kibiashara

Tovuti ya habari ya kituo cha Stand News itafungwa baada ya msururu wa upekuzi na watu kadhaa kukamatwa, operesheni iliofanyika Jumatano hii, Desemba 29, tovuti ya kituo hicho imetangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Stand News imetangaza kujiuzulu kwa mhariri mkuu wake Patrick Lam na kufukuzwa kazi kwa wafanyikazi wote. Tovuti haitasasishwa tena na inaonekana kuwa haitakuwa hewani hivi karibuni.

Jumla ya maafisa 200 wa polisi waliovalia sare na wengine waliovalia kiraia walishiriki katika operesheni ya asubuhi ya leo iliyolenga tovuti hii huru ya habari ya mtandaoni, tovuti ambayo kwa namna fulani ilikuwa imeziba pengo lililowekwa kwenye vyombo vya habari nchini kwa kufungwa kwa gazeti la kubwa la upinzani, Apple Daily, Juni mwaka jana.

Askari polisi wapatao 100 walifika eneo la tukio wakiwa na makumi ya masanduku makubwa ya plastiki kwa ajili ya kuhifadhi kompyuta na nyaraka, wafanyakazi waliokuwa katika ofisi za kituo cha Stand News waliamriwa kuondoka eneo la tukio na jengo likiwa limezingirwa.

Mtuhumiwa wa kula njama

Wakati huo huo takriban watu saba walikamatwa wakiwa majumbani kwao. Miongoni mwao ni mwimbaji maarufu wa pop na mwanaharakati wa demokrasia Denise Ho, ambaye alijiuzulu kutoka bodi ya wakurugenzi ya Stand News mwezi uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.