Pata taarifa kuu
HONG KONG-HAKI

Amnesty International yaondoka Hong Kong kwa hofu ya kufanyiwa mabaya

Shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Amnesty International limetangaza, Jumatatu, Oktoba 25, kuwa linafunga ofisi zake huko Hong Kong, likibaini kwamba "haiwezekani" kufanya kazi huko kwa uhuru kwa sababu ya sheria kali ya usalama wa kitaifa iliyowekwa mwaka jana na Beijing.

Amnesty International imetangaza kwamba inafunga ofisi zake Hong Kong kutokana na vitisho dhidi ya wafanyakazi wake kuhusu sheria ya usalama wa kitaifa Hong Kong.
Amnesty International imetangaza kwamba inafunga ofisi zake Hong Kong kutokana na vitisho dhidi ya wafanyakazi wake kuhusu sheria ya usalama wa kitaifa Hong Kong. ANTHONY WALLACE AFP/File
Matangazo ya kibiashara

"Uamuzi huu, uliochukuliwa, unatokana na sheria ya usalama wa kitaifa ya Hong Kong, ambayo inafanya kuwa haiwezekani kwa mashirika ya haki za binadamu huko Hong Kong kufanya kazi kwa uhuru na bila hofu ya kufanyiwa mabaya kutoka upande wa serikali," Anjhula Mya Singh Bais, mkuu wa shirika hilo akinukuliwa na shirika la habari la AFP amesema katika taarifa.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu - Amnesty International limesema sheria ya usalama wa kitaifa ya Hong Kong imeangamiza uhuru wa watu na kutengeneza hali ya dharura ya haki za binaadamu.

Sheria hiyo kali ya usalama wa kitaifa, ambayo inafanya kuwa uhalifu kitu chochote ambacho mamlaka zitakiona kuwa cha kuhujumu serikali, kutaka kujitenga, kula njama na mataifa ya kigeni na ugaidi ikiwa na adhabu ya kifungo cha maisha ya jela -- imebadilisha pakubwa mazingira ya kisiasa na kisheria ya Hong Kong.

Beijing ilisisitiza kuwa sheria hiyo ilihitajika kurejesha utulivu baada ya maandamano makubwa na wakati mwingine yenye vurugu ya kudai demokrasia mwaka wa 2019 lakini ikaahidi kuwa itawalenga tu wenye itikadi kali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.