Pata taarifa kuu
HONG KONG-HAKI

Hong Kong: Jimmy Lai ahukumiwa kifungo kipya

Tajiri na mmiliki wa vyombo vya habari Hong Kong Jimmy Lai ni miongoni mwa wanaharakati wanane wanaounga mkono demokrasia ambao wamehukumiwa leo Ijumaa kifungo kingine cha miezi kumli na nne kwa kushiriki katika maandamano yaliyopigwa marufuku siku ya kumbukumlbu ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa China ya Kikomunisti.

Tajiri na mmiliki wa vyombo vya habari Hong Kong Jimmy Lai.
Tajiri na mmiliki wa vyombo vya habari Hong Kong Jimmy Lai. ANTHONY WALLACE AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Bwana Lai, ambaye tayari yuko kizuizini kwa kushiriki katika mikutano mingine, alihukumiwa kifungo cha miezi 14 gerezani kwa kuandaa na kushiriki maandamano Oktoba 1, 2019. Kwa hivyo atalazimika kutumikia miezi 20 kwa jumla.

Viongozi wengine saba katika harakati za kupigania demokrasia, ikiwa ni pamoja na Figo Chan, mwanaharakati wa miaka 25, na wabunge wa zamani Lee Cheuk-yan na Leung Kwok-hung pia wamepewa hukumu mpya.

Walipofika mahakamni kwa gari la polisi, washtakiwa kadhaa walifanya ishara ya V kwa vidole kama ushindi.

Watu waliokuja kuwaunga mkono wameimba kwa maneno "ongeza mafuta", maneno ambayo hutumika sana Hong Kong kusaidia na kumtia moyo mtu aliye katika hatari.

Hukumu hizi zinaonyesha tena ukandamizaji wa China usiokoma katika eneo la Hong Kong.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.