Pata taarifa kuu
HONG KONG

Mwanaharakati wa Hong Kong Joshua Wong ahukumiwa kifungo cha ziada cha miezi 10

Joshua Wong, mtu mashuhuri katika harakati za demokrasia huko Hong Kong, atalazimika kutumikia kifungo cha miezi kumi gerezani kwa kushiriki mkutano wa hadhara bila idhini mnamo Juni 4, 2020.

Joshua Wong, ambaye ni mwanafunzi alipata umaarufu mkubwa baada ya kuongoza maandamano makubwa mwaka 2014 kushinikiza uongozi wa Hong Kong kukubaliwa wakaazi kupewa nafasi ya kuwachagua viongozi wao.
Joshua Wong, ambaye ni mwanafunzi alipata umaarufu mkubwa baada ya kuongoza maandamano makubwa mwaka 2014 kushinikiza uongozi wa Hong Kong kukubaliwa wakaazi kupewa nafasi ya kuwachagua viongozi wao. Anthony WALLACE AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mwanaharakati huyo kijana, mwenye umri wa miaka 24, tayari yuko gerezani kwa sababu ya hukumu zingine kwa makosa ya  kukusanyika kinyume cha sheria na ambaye ni mmoja wa wanaharakati 47 walioshtakiwa chini ya sheria mpya ya usalama wa kitaifa katika jijini hilo, amehukumiwa Alhamisi namahakama ya wilaya.

Hukumu yake ya miezi 15 imepunguzwa hadi miezi 10 kutokana na kosa alilolifanya.

Mwaka 2019, Joshua Wong aliachiliwa huru baada ya kufungwa jela kutokana na harakati zake za kupanga maandamano dhidi ya uongozi wa eneo hilo mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.