Pata taarifa kuu
CHINA-EU-SIASA-USALAMA

EU yalaani mpango wa marekebisho kwa uchaguzi wa Hong Kong

Umoja wa Ulaya umeshutumu muswada unaohusiana na marekebisho katika mfumo wa uchaguzi huko Hong Kong, mpango ambao unakiuka ahadi zilizotolewa za kulinda hadhi ya kujitawala ya jiji hilo kwa kuweka sheria za kibabe kutoka China,Umoja wa Ulaya umebaini

Katika hotuba yake ya ufunguzi katika kikao cha kila mwaka cha Bunge la China, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang ametoa ripoti ya mwaka uliopita na kutangaza yale yanayotakiwa kutekelezwa mwaka wa 2021.
Katika hotuba yake ya ufunguzi katika kikao cha kila mwaka cha Bunge la China, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang ametoa ripoti ya mwaka uliopita na kutangaza yale yanayotakiwa kutekelezwa mwaka wa 2021. REUTERS - CARLOS GARCIA RAWLINS
Matangazo ya kibiashara

"Marekebisho kama haya yanaweza kuwa na athari mbaya kwa kanuni za kidemokrasia na wawakilishi waliochaguliwa kidemokrasia huko Hong Kong. Pia mpango huo unaweza kupingana na marekebisho ya hivi karibuni ya uchaguzi huko Hong Kong na kurudi kwenye ahadi zilizotolewa," Umoja wa Ulaya umesema katika taarifa.

"Umoja wa Ulaya uko tayari kuchukua hatua zaidi kukabiliana na kuzorota zaidi kwa uhuru wa kisiasa na haki za binadamu huko Hong Kong, hali ambayo itakuwa kinyume na uwajibikaji wa China ndani na kimataifa," Umoja wa Ulaya umeongeza.

China inatarajiwa kuwasilisha katika kikao cha kila mwaka cha Bunge la taifa lmarekebisho ya mfumo wa uchaguzi huko Hong Kong ambayo inaweza kuimarisha sheria zake katika mji huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.