Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-SIASA-USALAMA

Bunge la China kuahirisha uchaguzi wa wabunge Hong Kong

Uchaguzi wa wabunge katika jimbo linalojitawala la Hong Kong huenda ukaahirishwa kwa mwaka wa pili hadi Septemba 2022, wakati Beijing inapanga kufanya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi wa jiji hilo.

Bunge la  China, linalokutana kuanzia Machi 5, 2021 kwa kikao chao cha kwanza cha mkutano wa kila mwaka, linatarajia kujadili kuhusu mageuzi ya mfumo wa uchaguzi Hong Kong.
Bunge la China, linalokutana kuanzia Machi 5, 2021 kwa kikao chao cha kwanza cha mkutano wa kila mwaka, linatarajia kujadili kuhusu mageuzi ya mfumo wa uchaguzi Hong Kong. REUTERS - CARLOS GARCIA RAWLINS
Matangazo ya kibiashara

Likinukuu vyanzo visivyojulikana, shirika la habari la South China Morning Post na vymbo vingine vya habari nchini China vimeripoti kuahirishwa kwa uchaguzi huo, ambao itakuwa sehemu ya mabadiliko yaliyoamuliwa na mamlaka ya China kuhusu muundo wa kisiasa wa Hong Kong.

Mabadiliko hayo yanatarajiwa kupitishwa katika Bunge la taifa ambalo litaanza shughuli zake leo Ijumaa na linatarajiwa kudumu wiki moja.

Wang Chen, mafisa wa China, ametangaza kuwa China itabadilisha saizi, muundo na utaratibu wa kuunda kamati ya uchaguzi ikimteua kiongozi wa Hong Kong na kumpa mamlaka ya kuteua wabunge wengi wa jiji hilo.

Wanasiasa wengi na wanaharakati wanaounga mkono demokrasia wako gerezani au uhamishoni baada ya mamlaka kuzima maandamano dhidi ya serikali mnamo mwaka 2019, na kuwekwa sheria mpya ya usalama wa kitaifa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.