Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-HAKI-SIASA

Kesi ya wanaharakati wanaotetea demokrasia Hong Kong kusikilizwa

Maelfu ya watu wamekusanyika nje ya mahakama ya Hong Kong Jumatatu hii kabla ya kusikilizwa kwa wanaharakati 47 wanaounga mkono demokrasia walioshtakiwa kwa madai ya kula njama ya kufanya uasi, wakati upinzani ukiendelea kukandamizwa na mamlaka chini ya sheria ya usalama wa kitaifa.

Profesa Benny Tai, mmoja wa wanaharakati 47 wanaotetea democrasia wanaoshikiliwa Hong Kong.
Profesa Benny Tai, mmoja wa wanaharakati 47 wanaotetea democrasia wanaoshikiliwa Hong Kong. ISAAC LAWRENCE AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati wanashutumiwa kwa kuandaa na kushiriki katika "uchaguzi wa mchujo" usiyo rasmi mwezi Julai 2020 ili kuteua wagombea wa kutoka kambi ya wanaharakati wanaounga mkono demokrasia kwa uchaguzi wa wabunge, ambao uliahirishwa na serikali ikibaini kuwa ni kutoakana na mgogoro wa kiafya unaosababishwa na virusi vya Corona.

Walishtakiwa Jumapili chini ya sheria ya usalama wa kitaifa iliyopitishwa mwaka jana, ambayo inaadhibu kile China inaeleza kwa upana kama vitendo vya uasi, kujitenga, ugaidi na ushirikiano wowote na mataifa ya kigeni.

Hong Kong kwa sasa iko chini ya ulinzi mkali, vikosi vya usalama vimewekwa katika maeneo mbalimbali, hasa kaibu na mahakama ya West Kowloon ambapo kesi hiyo itasikilizwa, na zaidi ya maafisa 100 wa polisi wamepelekwa wakati wafuasi wa wanaharakati wanaotetea demokrasia walimiminika katika moja ya mikutano mikubwa zaidi tangu kuanza kwa janga la Corona.

Foleni ndefu, iliyonyooka kwa mita mia kadhaa, imeshuhudiwa mbele ya mlango wa jengo hilo. Wanadiplomasia kadhaa wa kigeni walikuwa mwa umati wa watu hao.

Wengine wamesikika wakiimba nyimbo maarufu wakati wa maandamano dhidi ya serikali ya maka 2019 katika mkoa Maalum wa Utawala wa China, kama "Muiachilie Hong Kong" na "Tupiganie Uhuru".

Hapo awali, mamlaka zilionyesha kwamba kufanya kampeni kwa kupata idadi kubwa ya viti katika Baraza la Kutunga Sheria - bunge lenye viti 70 - kwa lengo la kuzuia mapendekezo ya serikali na kushinikiza mageuzi ya kidemokrasia kunaweza kutazamwa kama kitendo cha uasi.

Kesi hiyo inaashiria kikwazo kingine kwa harakati ya kupigania demokrasia, kwani maafisa kadhaa waliochaguliwa wamekataliwa na wanaharakati wengi walikamatwa tangu sheria ya usalama wa kitaifa ilianza kutekelezwa mwezi Juni mwaka jana, wakati wanaharakati wengine wamekimbilia nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.