Pata taarifa kuu
HONG KONG

Sheria kuhusu uhamiaji yatia hofu kwa uhuru wa kusafiri Hong Kong

Bunge la Hong Kong linajadili leo Jumatano mswada wenye utata kuhusu uhamiaji ambao umezua hofu kwa wanasheria, wanadiplomasia na wanaharakati kwamba mamlaka itakuwa na mamlaka kamili ya kuzuia wakaazi na wengine kusafiri kwenda au kuondoka katika jimbo hilo maalum la utawala wa China.

Moja ya vikao vya Baraza la Bunge Hong Kong, China, Aprili 8, 2021.
Moja ya vikao vya Baraza la Bunge Hong Kong, China, Aprili 8, 2021. REUTERS - TYRONE SIU
Matangazo ya kibiashara

Serikali katika jimbo la Hong Kong limziita hofu hizi kama "upuuzi mtupu", akisema mswada huo unakusudia kuzuia uhamiaji haramu na hauhusu haki ya kikatiba ya uhuru wa kutembea au kusafiri.

Lakini kauli hii ya viongozi wa Hong Kong  aileti faraja yoyote kwa wakaazi wa mji huo ambao wengi wanaona kwamba ni udikteta ambao unaendelea katika jimbo hilo tangu Beijing ilipoweka sheria mpya ya usalama wa kitaifa katika msimu uliyopita wa majira ya joto, sheria ambayo ilikosolewa na upinzani unaounga mkono Demokrasia.

Muswada huo unajadiliwa kwa mara ya pili na Baraza la Bunge, ambalo linaweza kupiga kura wakati wa mchana. Serikali haijakabiliwa na upinzani tangu wabunge wanaotetea Demokrasia kujiuzulu kwa wingi mwaka jana kupinga kufukuzwa kwa wenzao kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.