Pata taarifa kuu
HONG KONG

Maandamano makubwa Hong Kong 2019: Waandaaji wapatikana na hatia

Maveterani tisa wa upinzani katika jimbo la Hong Kong wamepatikana na hatia leo  Alhamisi ya kuandaa moja ya maandamano makubwa zaidi ya mwaka 2019, uamuzi ambao unaonyesha tena ukandamizaji mkali katika jimbo hilo la China.

Mwanaharakati anayeunga mkono demokrasia Lee Cheuk-yan anazungumza na wanahabari wakati akiwasili katika mahakama ya Magharibi ya Kowloon kuja kusikiliza hukumu katika kesi inayomkabili, huko Hong Kong, China Aprili 1, 2021.
Mwanaharakati anayeunga mkono demokrasia Lee Cheuk-yan anazungumza na wanahabari wakati akiwasili katika mahakama ya Magharibi ya Kowloon kuja kusikiliza hukumu katika kesi inayomkabili, huko Hong Kong, China Aprili 1, 2021. REUTERS - TYRONE SIU
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya watu wanaoheshimiwa sana katika kupigania uhuru katika eneo hili lililotawaliwa katika enzi za ukoloni na Uingereza, mara nyingi watetezi wa amani ambao kwa miongo kadhaa wamekuwa wakitetea watu washirikishwe katika uchaguzi wa viongozi wao, ni miongoni mwa watu hao tisa.

Mmoja wa watu hao mashuhuri ni wakili Martin Lee, 82, ambaye kabla ya kutaka kujitenga kwa eneohilo mwaka 1997 aliteuliwa na Beijing kuandaa Sheria ya Msingi, ambayo hutumika kama katiba ndogo katika eneo hilo linalojitawala.

Wengine walioshtakiwa ni mbunge wa zamani wa upinzani na wakili Margaret Ng, 73, mkuu wa vyombo vya habari Jimmy Lai na mbunge wa zamani Leung Kwok-hung anayejulikana kwa jina la utani "Long Hair".

Watu wawili maarufu wazuiliwa jela

Wawili kati ya viongozi hao wanaokabiliwa na kifungo cha miaka mitano, kwa sasa wako kizuizini kwa mashtaka tofauti chini ya sheria kali ya usalama wa kitaifa ambayo Beijing iliweka mnamo mwezi Juni.

Wengine ni viongozi  kutoka mashirika ya kiraia, Civil Front for Human Rights (CHRF), muungano ambao uliandaa maandamano makubwa mnamo mwaka 2019, wakati jiji lilipokumbwa na mzozo mbaya zaidi wa kisiasa tangu mwaka 1997.

Wawili kati ya tisa wakiri kosa

Mahakama ya Wilaya ya Hong Kong iliwapata saba na hatia ya kuandaa na kushiriki katika mkusanyiko haramu. Wengine wawili walikiri kosa.

Tisa wote, ambao wanakabiliwa na kifungo cha miaka mitano gerezani, watafahamishwa kifungo chao tarehe 16 Aprili. Washtakiwa ambao hawajazuiliwa wameachwa huru, kwa sharti kwamba warudishe hati zao za kusafiria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.