Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

China: Tajiri kutoka Canada ahukumiwa kifungo cha miaka kumi na tatu jela kwa ulaghai

Tajiri wa Canada mwenye asili ya China, Xiao Jianhua, ambaye alitoweka mnamo 2017 kutoka hoteli moja huko Hong Kong, amehukumiwa kifungo cha miaka kumi na tatu jela, vyombo vya shria vimetangaza Ijumaa Agosti 18. Xiao Jianhua alipokamatwa alikuwa mmoja wa watu tajiri zaidi nchini China, mwenye utajiri unaokadiriwa dola bilioni sita.

Tajiri wa Canada mwenye asili ya China Xiao Jianhua, ambaye alitoweka kutoka hoteli moja huko Hong Kong mnamo 2017, alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela.
Tajiri wa Canada mwenye asili ya China Xiao Jianhua, ambaye alitoweka kutoka hoteli moja huko Hong Kong mnamo 2017, alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela. La Universidad China de Hong Kong/AFP
Matangazo ya kibiashara

Xiao Jianhua alipatikana na hatia ya "ubadhirifu wa fedha za umma" na "matumizi haramu ya fedha", imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari Mahakama ya Shanghai, ambapo mfanyabiashara huyo amehukumiwa.

Kutoweka kwake mnamo 2017 kulizua taharuki huko Hong Kong. Xiao Jianhua anayedaiwa kuwa na ushirika wa karibu na viongozi wakuu wa Kikomunisti wa China, kulingana na ripoti za vyombo vya habari, alitekwa nyara na maafisa wa Beijing. Tangu wakati huo, habari ndogo ilikuwa imevuja kuhusu kesi hiyo na viongozi wa China walikaa kimya.

Kampeni ya kupambana na rushwa yazinduliwa mwaka wa 2012

Uchunguzi dhidi ya Xiao Jianhua unaonekana kuwa sehemu ya kampeni kubwa ya kupambana na ufisadi iliyoanzishwa na Rais wa China Xi Jinping alipoingia madarakani mwaka 2012. Tukio la kutekwa nyara kwa Xiao Jianhua huko Hong Kong lilitokea wakati ambapo maafisa kutoka China bara hawakuruhusiwa kufanya hivyo katika eneo la linalojitawala.

Wakati huo, baadhi ya watu walihofia kwamba wakazi wa jiji hilo waliweza kupelekwa kwa nguvu hadi China Bara, ambako mahakama kwa kiasi kikubwa zinategemea Chama tawala cha Kikomunisti. Hofu hizi zilikuwa kiini cha maandamano ya kuunga mkono demokrasia ambayo yalitikisa Hong Kong mnamo 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.