Pata taarifa kuu

Hong Kong: Kardinali Zen kufikishwa mahakamani, uhusiano kati ya China-Vatican mashakani

Kesi ya Kadinali Joseph Zen itafunguliwa Jumatatu hii, Septemba 19 huko Hong Kong. Akiwa na umri wa miaka 90, askofu huyo mstaafu atafikishwa mahakamani pamoja na washtakiwa wengine wanne ambao waliunga mkono waandamanaji wanaounga mkono demokrasia kisiwani Hong Kong. 

Kardinali Zen wakati wa misa huko Hong Kong mnamo Mei 24, 2022.
Kardinali Zen wakati wa misa huko Hong Kong mnamo Mei 24, 2022. AP - Kin Cheung
Matangazo ya kibiashara

Ni diplomasia ya mazungumzo kati ya China na Papa Francis ambayo inawekwa kwenye majaribio katika kesi hii. Kesi hii inakuja huku makubaliano ya siri ya kila mwaka yaliyofikiwa mwaka 2018 kati ya Beijing na Vatican, ambayo yanaidhinisha Chama cha Kikomunisti cha China kuwateua maaskofu kwa idhini ya Holy See, yatafanywa upya. Joseph Zen alikuwa kinyume na kile anachokiona kama "kuchafua Kanisa" na tishio kwa mapadre wa Kanisa za siri nchini China.

Adui wa Beijing

Tulikutana naye mnamo Septemba 2019, wakati wa maandamano dhidi ya sheria ya sheria maalumu ya usalama wa kitaifa iliyowekwa na Beijing huko Hong Kong. Askofu mkuu wa zamani aliyeteuliwa na John Paul II alikuwa tayari amestaafu. Hii haikumzuia kueleza kutokubaliana kwake kwa nguvu, na Vatican kulegeza msimamo wake. Wakati huo aliiona Roma ikiwa mbali sana na vuguvugu linalotetea demokrasia  Hong Kong. “Makao makuu ya Kanisa Katoliki haijasema neno lolote kuhusu vuguvugu hili. Hii ni ishara mbaya sana. Wanatetea usawa. Haina maana! Kwa sababu tayari tuko na msimamo wetu. Ni serikali na polisi wanaodhulumu. Ninasikitika kuyasema haya, lakini kanisa limegawanyika. »

Tofauti ndani ya Kanisa ambazo zinaweza kuwa zilisumbua wengine kwenye makao maku ya Kanisa Katoliki na kumfanya Joseph Zen kuwa adui wa mamlaka ya China. Ili kutoharibu uhusiano mpya kati ya chama tawala cha CCP na Vatican yakikaribia maandalizi ya Kongamano la 20 la chama tawala mwezi ujao, adhabu dhidi ya Askofu huyo imepunguzwa. Alipokamatwa Mei 11 chini ya sheria mpya ya usalama wa taifa, Joseph Zen alishutumiwa kwa mara ya kwanza kwa kusimamia Mfuko wa Misaada wa Kibinadamu wa "6.12", uliokusudiwa kutoa msaada wa kifedha kwa waandamanaji wanaoipinga serikali huko Hong Kong, kuwaruhusu hasa kulipa mwanasheria au kutafuta matibabu.

Lakini kesi hii inaendelea kutatiza uhusiano kati ya China na Vatican. Wakati wa safari yake rasmi nchini Kazakhstan wiki iliyopita, rais wa China alikataa pendekezo la mkutano na Papa Francis, ambaye pia alikuwa katika ziara huko Asia ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.