Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa urais Indonesia: Prabowo Subianto adai 'ushindi katika duru ya kwanza'

Raia wa Indonesia wamechagua wabunge 580 na wawakilishi 20,000 wa kikanda na wa ndani mnamo Februari 14. Lakini ni juu ya uchaguzi wote wa urais ambao umevutia umakini katika nchi hii ya tatu inayochukuliwa kuwa yenye demokrasia thabiti ulimwenguni kwa idadi ya wakaazi. Matokeo rasmi hayatatangazwa hadi Machi 2024, lakini tayari makadirio ya kwanza yameanza kutolewa.

Indonesian presidential candidate Prabowo Subianto salutes as he waits for his turn to vote at a polling station during the election in Bojong Koneng, Indonesia, Wednesday, Feb. 14, 2024.
Waziri wa Ulinzi Prabowo Subianto (picha yetu) amedai, Jumatano, Februari 14, "ushindi katika duru ya kwanza" wakati wa uchaguzi wa urais nchini Indonesia. AP - Vincent Thian
Matangazo ya kibiashara

 

Ni lazima tuwe waangalifu, asema mwandishi wetu wa habari huko Jakarta, Juliette Pietraszewski, lakini tunaelekea kwenye uongozi mkubwa wa Prabowo Subianto, Waziri wa Ulinzi ambaye hapo zamani alizua gumzo. Hata kama amedai ushindi kumrithi Joko Widodo mwezi Oktoba mwaka huu katika uongozi wa nchi hii ya tatu yenye demokrasia thabiti duniani, jenerali huyo wa zamani amebaini kwamba atasubiri "matokeo rasmi" ya tume ya uchaguzi. "Tunaamini kuwa demokrasia ya Indonesia inafanya kazi vizuri. Wananchi wameamua, wananchi wameamua,” amewaambia waandishi wa habari, kabla ya kutoa wito wa umoja.

Subira

Tahadhari, na juu ya yote subira, pia ni hotuba za wagombea wengine wawili. Ganjar Pranowo, gavana wa zamani wa Java ya Kati, ambaye alikuwa wa mwisho katika makadirio kulingana na sampuli, ametoa wito wa kusubiri matokeo rasmi kutoka kwa KPU. KPU [Tume Kuu ya Uchaguzi] ndiyo tume inayohusika na uchaguzi mkuu. Kinachopaswa kueleweka ni kwamba ikiwa makadirio ya kwanza ya uchaguzi huu yatawasilishwa, matokeo rasmi yatatangazwa baadaye, ndani ya muda wa siku 35. Yanatarajiwa katikati ya mwezi Machi. Wakati huo huo, lazima tuwe watulivu na wavumilivu kwa sababu kila kitu bado kinaendelea, walitangaza baadhi ya wafuasi wa mgombea Ganjar.

Hotuba nyingine jioni hii, ya kambi ya Anies Baswedan, gavana wa zamani wa Jakarta, mgombea ambaye, kulingana na makadirio ya awali, yanazunguukia kwa karibu 25%. Kambi ya Anies Baswedan pia imesema inasubiri matokeo rasmi. Pia imetaja kuwa na "ripoti nyingi zinazopendekeza udanganyifu," lakini bila kutoa maelezo zaidi.

Kauli za utaifa

Ikiwa makadirio ya sasa yatathibitishwa rasmi na KPU, basi Prabowo Subianto atakuwa rais mteyle wa Indonesia na makamu wake atakuwa si mwingine bali Gibran, mtoto wa rais wa sasa Joko Widodo.

Mgombea kwa mara ya tatu, Bw. Prabowo ameendeleza matamshi ya utaifa na watu wengi na kuahidi kuendeleza sera za rais anayeondoka madarakani. Wagombea wengine na vuguvugu la wanafunzi walimshutumu rais anayemaliza muda wake, Joko Widodo, kwa kutumia rasilimali za serikali kujaribu kushawishi uchaguzi kwa ajili ya waziri wake. Akiwa mkuu wa kikosi maalum, Bw Prabowo alishutumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kuamuru kutekwa nyara kwa wanaharakati wanaounga mkono demokrasia katika miaka ya 1990, kuelekea mwisho wa utawala wa Suharto. Alikanusha mashtaka haya na hakuwahi kufunguliwa mashtaka.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.