Pata taarifa kuu

Kumi na moja wafariki katika mlipuko wa volkano ya Marapi, magharibi mwa Indonesia

Takriban wapanda mlima kumi na moja wamepatikana wamekufa kufuatia mlipuko wa volkano magharibi mwa nchi, afisa wa uokoaji wa eneo hilo amesema Jumatatu.

Indonesia ina karibu volkano 130 hai.
Indonesia ina karibu volkano 130 hai. REUTERS/Karolus Naga
Matangazo ya kibiashara

Volkano ya Marapi ambayo inapatikana kwenye kisiwa cha Sumatra, ililipuka siku ya Jumapili. Takriban Wapanda mlima 11 wamepatikana wamekufa.

"Kuna watu 26 ambao hawakuhamishwa, tulipata watu 14, watatu walipatikana wakiwa hai na 11 walipatikana wamekufa," Abdul Malik, mkuu wa shirika la utafutaji na uokoaji la Padang, amesema siku moja baada ya mlipuko huo.

Mlipuko wa Mlima Marapi, katika kisiwa cha Sumatra, ulianza Jumapili alasiri. Abdul Malik amesema kulikuwa na jumla ya wapanda mlima 75 ambao walikuwa kwenye mlima tangu Jumamosi na waokoaji walikuwa wakijaribu kuwahesabu.

"Mlima wa Moto"

Kumi na wawili kati yao bado hawajapatikana na 49 wameshuka kutoka mlimani, wengine wamepelekwa hospitalini.

Majivu yaliyotolewa kutoka Mlima Marapi yalionekana hadi mita 3,000 juu ya kilele chake, Hendra Gunawan, mkuu wa Kituo cha Indonesia cha Vulcanology na Hatari za Jiolojia, alisema siku ya Jumapili.

Vikosi vya uokoaji vilifanya kazi usiku kucha kusaidia wapanda mlima kufika mahali salama, Shirika la Uhifadhi wa Maliasili la Sumatra Magharibi limesema. Rudy Rinaldi, mkurugenzi wa shirika la kukabiliana na maafa la Sumatra Magharibi, amesema baadhi ya wapanda mlima waliokolewa walikuwa wakipokea matibabu.

"Wengine waliungua kutokana na joto kali na walipelekwa hospitalini," amesema. "Waliojeruhiwa ni wale waliokaribia kreta."

Marapi, yenye urefu wa mita 2,891 na ambayo jina lake linamaanisha "mlima wa moto", ni volkano hai zaidi katika Sumatra. Kulingana na mamlaka, kwa sasa iko katika ngazi ya tatu ya tahadhari, kwa kiwango cha nne. Indonesia ina karibu volkano 130 hai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.