Pata taarifa kuu

Tanzania na Indonesia kuimarisha uhushirkiano katika sekta mbalimbali

Nairobi – Tanzania na Indonesia, zimekubaliana kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili katika sekta ya diplomasia, uchumu, afya na kilimo, na kutiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na mgeni  wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia  Joko Widodo
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Joko Widodo © ikulu ya Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Rais Widodo amewasili Jumatatu jijini humu, leo akihitisha ziara ya siku mbili amekutana na Mwenyeji wake Ikulu kwa mazungumzo ya faragha.

Mara baada ya mazungumzo hayo, nchi hizo zilisaini hati saba za makubaliano ya ushirikiano katika kilimo, Indonesia kuiuzia Tanzania dawa, Miongoni mwa mengine. 

Tanzania na Indonesia zinalenga kujiimarisha zaidi katika sekta mbalimbali
Tanzania na Indonesia zinalenga kujiimarisha zaidi katika sekta mbalimbali © ikulu ya Tanzania

Rais Samia anasema hatua hii inaimarisha uhusiano katika sekta mbalimbali.

“Tumekubaliana kwa pamoja kukuza biashara kwa kuzileta pamoja sekta za umma na binafsi na hapa tumelenga kushirikiana katika kilimo, viwanda, uwekezaji, Nishati Mafuta na gesi, Uvuni utalii na Sekta za Ukarimu, na kubadilishana maarifa na teknolojia. ” alieleza rais Samia.

00:14

Rais wa Tanzania Samia Hassan

Naye rais Widodo anasema uhusiano huu ulioasisiwa tangu mwaka 1955, una kila sababu ya kuimarika mara dufu hasa kwa kuongeza biashara baina ya nchi hizi

Indonesia inafanya juhusi ili kuingia Makubaliano ya kibiashara ili kuimarisha biashara baina ya nchi zet ambazo kwa mwaka 2022 biashara iliongezeka kwa asilimia 2.7 pia kuchakata gesi asilia kuwa bidhaa kamili kama mbolea. ” Alisema rais Joko Widodo.

00:20

Rais Widodo kuhusu ushirikiano na Tanzania

Tanzania huuza mazao nchini Indonesia yakiwemo karafuu,tumbaku, karanga pamoja na madini mbalimbali  huku Indonesia ikiiuzia Tanzania bidhaa za kemikali karatasi na nguo.

Tanzania na Indonesia zimetia saini makubaliano kati yake yanayolenga kuimarisha ushirikiano
Tanzania na Indonesia zimetia saini makubaliano kati yake yanayolenga kuimarisha ushirikiano © ikulu ya Tanzania

Steven Mumbi/Dar es salaam/Rfi Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.