Pata taarifa kuu

Thailand: 18 wuawa katika mlipuko wa kiwanda cha fataki

Mlipuko katika kiwanda cha fataki katikati mwa Thailand, katika jimbo la Suphanburi, umeua takriban watu 18, waokoaji wamesema Jumatano Januari 17, kulingana na shirika la habari la AFP.

Fataki zikifyatuliwa kwenye sherehe ya Marina Bay huko Singapore.
Fataki zikifyatuliwa kwenye sherehe ya Marina Bay huko Singapore. Reuters / Vivek Prakash
Matangazo ya kibiashara

 

Tunathibitisha vifo 18," mjumbe wa timu ya uokoaji aliye kwenye eneo la tukio ameliambia shirika la habari la AFP. Mlipuko huo ulitokea mchana, vyombo vya habari vya Thailand vimesema.

Picha zilizotolewa na waokoaji zinaonyesha eneo lililoharibiwa na mlipuko huo, ambapo ni baadhi ya vifusi tu vilivyosalia.

ripoti ambayo bado haina uhakika

Polisi imethibitisha vifo kadhaa kwa shirika la habari la AFP, lakini bila kuweka idadi ya watu waliouawa kwa sasa au kutoa maelezo zaidi.

"Hatujaona uharibifu mkubwa kwa nyumba nyingine au watu wanaoishi katika kijiji jirani," Theerapoj Rawangban, afisa wa polisi wa eneo hilo amesema.

Tukio kama hilo lilitokea mwezi wa Julai mwaka uiyopita huko Sungai Kolok, kusini mwa Thailand, ambapo mlipuko katika ghala la fataki uliwaua watu kumi na kujeruhi wengine zaidi ya mia moja.

Nchini Thailand, mashaka makubwa yanaendelea kuhusu kutofuata sheria za msingi za usalama, sababu ya matukio kadhaa mabaya katika miaka ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.